Msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kabla ya Masogange kujisalimisha mahakama ilitoa hati ya kumkamata baada ya kushindwa kuhudhuria mara mbili kwenye kesi hiyo inayomkabili.
Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange ilikuja baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakama kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshtakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.
Hivyo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata Masogange.
Hata hivyo, Masogange leo (Jumanne) amefika mahakamani hapo mapema.
Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.