Ilikuwa balaa leo alfajiri katika maeneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya tembo wanne kutinga chuoni hapo.
Watu wamefurika chuoni hapo kuwaangalia lakini polisi wamewazuia kusogea karibu na eneo walipo tembo hao.
Msemaji wa Tanapa, Paschal Shelutete amesema tayari wameshaita askari wa wanyapori kutoka Manyoni kwa ajili kuwaondoa tembo hao.
Shelutete amesema askari hao wanatarajiwa kufika wakati wowote kuanzia sasa.