Yanga imepata pigo lingine nchini Algeria baada ya wachezaji wake kuchelewa ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene, jijini Algers.
Wachezaji hao walikuwa wasafiri na ndege ya Uturuki kupitia Istanbul wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa walichelewa kufika uwanjani hapo.
Wakati benchi la ufundi na wachezaji wachecha wakiondoka leo, wachezaji waliochwa na ndege wanategemea kuondoka Algeria kesho au keshokutwa.
Yanga imeondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa mabao 4-0 na MC Algers katika mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Algeria.