Watu watatu wamenusurika kufa huku mamia ya abiria wanaosafri kuelekea Dar es Salaam na mikoa ya Lindi na Mtwara na wanaotokea mkoa wa Ruvuma wakielekea mikoa hiyo wakikwama njiani baada ya roli lililobeba makaa ya mawe aina ya Scania kupinduka na kuziba barabara katika daraja la Lwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
Walionusurika kwenye ajali hiyo akiwemo kondakta wa lori hilo lililotokea mkoani Ruvuma likielekea jijini Dar es Salaam Bw. Charles Ngonyani wanasema ajali hiyo imetokea wakati dereva wao haji mashaka akilikwepa lori jingine aina ya fuso ndipo likapinduka na kuziba barabara.
Kondakta huyo anasema kuwa katika ajali hiyo aliyeumia zaidi ni dereva wao Haji Mashaka aliyelazwa katika kituo cha afya cha Namtumbo huku yeye na mwenzake Charles Ngaponda wakipata majeraha madogo madogo.
Kwa upande wao abiria wanaosafiri kuelekea mikoa ya Dar es Salaam na mikoa ya Lindi na Mtwara na wanaotokea mkoa wa Ruvuma wakielekea mikoa hiyo wanaeleza adha wanayoipata kutokana na ajali hiyo.
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limethibitisha kutokea kwa ajali hiy huku likisimamia zoezi la kuliondo lori lililoziba bara bara.