Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime - SACP
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyekamatwa huko katika kijiji cha Nga’mbi kitongoji cha Mgaye Wilayani Mpwapwa akiwa a silaha tano (5) aina ya Gobore pamoja na zana za kutengenezea silaha za aina hiyo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwanandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema anayeshikiliwa ni BAHATI S/O MWANDACHE mwenye miaka 65, Mkaguru, Mkazi wa NGA’MBI.
Kamanda MISIME amesema mtu huyu ni mtengenezaji wa wa silaha za aina hiyo ambazo uchunguzi wa awali umebaini kuwa hutumiwa pia na wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo uwindaji haramu.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda MISIME anawashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoshirikiana na Jeshi la Polisi kuweza kuwafichua waharifu na kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu na wahalifu.