MAJAMBAZI wawili waliokuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili T 225 CQC aina ya Kapor wamekamatwa wakiwa na silaha wakijiandaa kufanya uhalifu katika kituo cha kuuza mafuta cha Oilcom kilichopo Kongowe-Mbagala, jijini Dar!
Majambazi hayo yametiwa mbaroni na askari polisi zaidi ya kumi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia wakiwa na magari aina ya Land Cruiser yenye namba za usajili T 148 AEN na T 848 AGF!