Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma (RPC), David Misime - SACP
Bangi zilizokamatwa katika msako huo uliofanywa na jeshi la polisi mkoani Dodoma.
Zana za kuvunjia zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma baada ya msako mkali
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu nane (8) waliokamatwa wakiwa na kilo moja na misokoto 104 ya bangi, zana za kuvunjia yakiwemo mapanga, mikasi, visu, nondo pamoja na mirungi gramu 500.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema mafanikio haya yametokana na msako unaoendelea Mkoani Dodoma wa kupambana na wahalifu na uhalifu uliofanyika eneo la Chang’ombe tarehe 11/03/2014 majira ya saa 01:00Hrs hadi 05:00Hrs na ulihusisha zaidi kero za uvutaji wa bangi na kupelekea kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali manispaa ya Dodoma.
Kamanda MISIME amewataja waliokamatwa katika msako huo kuwa ni:-
1. HALFANI S/O MUHEZA mwenye miaka 25, Mgogo, Mkulima.
2. STEWART S/O SYLVESTER mwenye miaka 18, Mgogo, Mkulima.
3. SHABAN S/O IBRAHIM mwenye miaka 18, Mgogo, Mkulima.
4. ABDALLAH S/O IDDI mwenye miaka 18, Mnyaturu, Mkulima.
5. FIKIRI S/O JONAS mwenye miaka 20, Mgogo Mkulima.
6. ALLY S/O NURU mwenye miaka 30, Mgogo, Mkulima
7. SAIMON S/O ZABRON mwenye miaka 43, Mchaga, Mkulima.
8. ALBERT S/O CHARLES mwenye miaka 18, Mgogo, Mkulima wote wakazi wa eneo la Chang’ombe, Manispaa ya Dodoma.
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kesho tarehe 12/03/2014 kujibu tuhuma zao zinazowakabili.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea kumtafuta Dereva wa gari linalosemekana kuwa ni TOYOTA LAND CRUISER GX STANDARD rangi nyeupe baada ya kumgonga mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la JULIAS S/O SANDUKU mwenye miaka 50, Mkaguru, Mkulima, Mkazi wa Gairo katika eneo la Kijiji cha Visimi Kibaigwa na kumsababishia kifo mpanda baiskeli huyo.
Kamanda MISIME amesema dereva huyo ambaye alikuwa anatokea Dodoma kuelekea uelekeo wa Mkoa jirani wa Morogoro baada ya kumgonga mpanda baiskeli huyo, alishuka kutoka ndani ya gari na kumwangalia aliyemgonga alipogundua amefariki akageuza gari kurudi njia ya Dodoma na kuwaambia wananchi waliojitokeza kuwa anaenda kutoa taarifa Polisi jambo ambalo hakufanya.
Kamanda MISIME amewaomba wananchi wenye taarifa na dereva huyo alipo wajulishe katika kituo chochote cha Polisi ili aweze kukamatwa.