Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UNATAFUTA KUPENDWA NA WALE WANAOKUZUNGUKA? BASI SOMA HAPA

$
0
0

Ni moja ya mawazo na fikra ndani ya watu wengi, kama hujawahi kuwa kwenye hali hiyo ninaweza kusema una bahati. Kwanini watu hawanipendi? Ni swali ambalo mara nyingi kila mtu hujaribu kujiuliza labda moja kwa moja au kwa kufanya vitu ili aweze kukubalika na watu fulani.
Inawezekana wewe ni mwandishi wa makala fulani, au mwimbaji, au mfanya biashara au mfanyakazi kama wengine , bosi, mfagiaji hata kama ni mlinzi. Kama ilivyo kwa mtu yeyote mimi pia ninapenda nipendwe, hiyo ni kibinadamu kabisa na hakuna tatizo kuhusu hilo. Tatizo ni pale unapotaka watu wakupende huku ukijaribu kufanya hiki na kile, sio kazi yako kumshawishi mtu akupende kama uko kazini au nyumbani, kwenye biashara na sanaa nyingine. Ukijikuta wewe unajaribu kushawishi watu ili upate marafiki, wafuasi, inawezekana hufanyi mambo yako sawasawa.
Badala ya kuwambia watu au kuwashawishi wakupende, zingatia kazi na majukumu yako, yafanye vizuri na kwa ustadi mkubwa. Utakapofanya kazi zako vizuri, mfano labda wewe ni mwandishi unahitaji kuandika makala zenye kuleta tija kwa wasomaji wako huku ukionyesha weledi wa hali ya juu au wewe ni mpishi wa mgahawa hapo mtaani unachotakiwa kufanya ni kupika chakula kizuri na kwa kuzingatia afya bora utajikuta watu wanakupenda na kuipenda kazi zako.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Hakuna bia utakazomnunulia mtu zinazoweza kumshawishi akupende, siku hizo bia zikiisha na yeye anaondoka, Si kwa kumtoa na kumpeleka kula hoteli nzuri au kwa kufanya vituko kujaribu kutafuta ushawishi watu wakupende. Pale unapojaribu kufanya watu wakupende ndipo unapoweza kujiharibia au kuharibu maisha yako na taaluma yako, fanya kitu sahihi na watu sahihi na mwishowe utapata watu sahihi wanaokupenda na kukuthamini.
Usijiunge na kundi fulani la watu ili uonekane unakubalika, bali fanya kinachostahili kufanywa na watu watakukubali. kwa kufanya hivyo utapotesha wanafiki wengi na kupata marafiki na watu wakweli wanaopenda kazi yako, jitihada zako na bidhaa zako. Kama unahitaji kung’ara utang’ara tu kwakuwa unafanya kitu sahihi.
Je unahitaji watu wakupende na kupenda kazi zako mwezi huu? Dumisha ubora wa kazi zako ikiwezekana ongeza ubora, fanya kazi kwa juhudi, kama ni mwanamuziki ungeza ubunifu katika kazi zako na usiambatane na watu wasiokua na tija kwenye taaluma yako.
Uwe na wiki njema yenye mafanikio.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>