Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo akiongoza dua ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemela akiongoza sala ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma. (PICHA NA HASSAN SILAYO)
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwaeleza jambo wajumbe wa Bunge maalum la Katiba Edward Lowassa (mwenyeshati Jeupe) na Philemon Ndesamburo, Ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti kuhusu Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, Mhe Profesa Costa Mahalu (kulia) akiteta na wajumbe wa kamati hiyo Bungeni Mjini Dodoma baada ya Semina ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kuahirishwa hadi kesho saa nne.
Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akiteta na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe James Mbatia kwenye ukumbi wa bunge Mjini Dodoma baada ya Semina ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kuahirishwa hadi kesho saa nne.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo wajumbe wenzie Bi. Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Richard Ndassa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, kabla ya kuingia katika Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli akimweleza jambo Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw. John Mnyika Mapema leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Ismail Aden Rage (mwenye kanzu) na Hashim Rungwe wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo Mjini Dodoma