Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

JIKO LA GESI LATEKETEZA NYUMBA MISUNGWI MKOANI MWANZA

$
0
0
Mwananchi akiwa juu ya paa la nyumba ya mtu mmoja maarufu kwa jina la Mama Mayunga, akijaribu kurusha vifuko vya mchanga katika moja ya majengo ya nyumba iliyozuka moto Jana majira ya saa 5 asubuhi mtaa wa Majengo jirani na Masangwa Guest House wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Moto huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake.

 ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
Moto ukipamba moto na kutokea kwenye madirisha ukivuma.
Ingawa jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuwasihi wananchi kusogea mbali toka eneo la moto kwani chanzo chake ni moto wa gesi katu watu hao hawakutii amri hiyo zaidi ya kuusogelea zaidi.
Saa moja baadaye gari la zimamoto lilifika eneo la ajali ya moto lakini hata hivyo liliambulia kuzima magofu huku milango, madirisha na mali zilizokuwa kwenye nyumba hiyo zikiteketea kabisa.
Hali ndiyo ilivyokuwa huku wananchi hao wa wilaya ya Misungwi wakisubiri huduma ya zimamoto toka magari ya Halmashauri ya jiji la Mwanza, umbali wa dakika 45.
Hali tete.(Picha :Wiliam Bundala wa matukiodaima.com kanda ya Ziwa)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>