Kampuni ya LG ya Korea Kusini imetoa simu mpya LG G Flex zilizotengenezwa kwa material yanayoziwezesha simu hizo kurudi katika hali yake ya upya, hata baada ya kupata mikwaruzo ya kawaida ambayo hufanya simu ionekane kuchakaa. Simu hizo zina uwezo wa kujirudisha katika hali ya kawaida (self-healing) mara baada ya kupata mikwaruzo ya kitu chenye ncha kama funguo, kisu nk, na baada ya muda alama zote za mikwaruzo zinapotea na kurudi ilivyokuwa.
Pia display ya simu hizo za LG G Flex imetengenezwa kwa plastic badala ya kioo kama zilivyo simu zingine, na pia muundo wake wa kujikunja (curve) unairuhusu simu kunyooka pindi inapokandamizwa kwa nguvu na kurudi katika hali yake bila kuvunjika.
Kwa simu hizi za G Flex, mtumiaji hatapata yale maumivu ambayo huwakuta watumiaji wengi ya kuvunjika kwa kioo, au simu kupata mikwaruzo mingi inayosababisha kuifanya ichakae haraka.
GG Flex ambazo kwa sasa zinapatikana Korea peke yake zitazinduliwa kwa soko la kimataifa Jumanne ijayo (December 3) huko Hong Kong. Bei ya simu hizo kwa Korea ni 999,990KRW sawa na Tsh milioni moja na nusu.
Tazama video kujionea majaribio ya G Flex
SOURCE: YAHOO