Hawa nao wanauza Viatu pande hizi kwa bei nafuu...
Wengine wanauza samaki katika eneo ambalo kiafya sio sahihi
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUOFYA HAPA CHINI
Wenye kuuza Nguo za ndani katika eneo kama hili nao wapo ingawa napo kiafya sio nzuri yaweza sababisha magonjwa ya ngozi kwa sababu watu wengi wanaonunua huishia kuvaa moja kwa moja bila hata kufua
Hawa wametundika Suluali pembezoni mwa Barabara
Eneo hili lina vumbi na huku wakiwa wameanika T-Shirt zao na kuuza kitendo kinacho sababisha kupatwa vumbi na kuhatarisha afya za watumiaji.
Wengine wanauza Urembo pamoja na makasha ya simu
Hii kali sana hawa Jamaa wanauza DVD kwa Tsh 500 hadi 1,000 bei ya juu sasa swali linakuja hapa kuna kazi za Nje na ndani ya Tanzania Je Haki miliki Mpo? na watu wa mapato hili mnalionaje?
Wauza Radio kwa Bei nafuu sana nao wapo
Huu ni uzibe wa Barabara kuu na wapita kwa miguu lakini vya kuzibia vimejaa nguo mbalimbali je Hiyo ni sehemu halali ya kufanyia Biashara?
Katika eneo hili la Ubungo sio pembezoni mwa barabara pekee lakini hadi mabondeni biashara zinaendelea kwa kasi.
Hawa nao wapo wanauza Vioo vya kujitazamia pamoja na vifaa vya kuegeshea nguo
Mikanda ya nguo mbalimbali nayo inauzwa katika eneo hili
Miwani ya wakubwa na watoto nayo ipo kwa bei poa
Ma bukta yakutosha yanauzwa eneo hili , yakiwa yamepigwa vumbi la kutosha
Hii ndiyo hali Halisi ya eneo kutoka Ubungo Darajani karibia na mitambo ya Gesi hadi eneo la watu wanaopandia magari ya kwenda Mwenge. Je Halmashauri ya Jiji hamlioni hili? Je Manispaa husikia nanyie hamlioni hili? Au hili ni eneo halali limepitishwa kwa ajili ya kufanya biashara hizi?
Hili ni eneo la Ubungo ambapo Kumekuwa na kero kubwa ya wafanya bishara wadogo wadogo kuegesha biashara zao za kila aina pembezoni mwa njia za wapita kwa miguu jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji hao wa barabara hiyo.
Licha ya usumbufu huo na kero hiyo, eneo hilo kutokana na msongamano wa watu wengi sana, limekuwa ndio maskani kwa vibaka ambao hujipatia kipato chao bila hata ya jasho kwa kujichanganya humo kama raia wa kawaida na kufanya wizi.
Wakizungumza watumiaji mbalimbali wa barabara hiyo wamelilalamikia Jiji na Manispaa husika kwa kushindwa kuwataftia eneo husika wafanyabiashara hao wadogo wadogo na kwamba kutokana na uzembe huo mkubwa wakuto wazuia nao wameamua kuendelea kuleta kero
"Eneo hili kwa kweli linatia Aibu sana kwa sababu hapa ndipo Lango kuu la kuingia jijini na mara watu wanapo ingia wanakutana na kero hii ambayo mimi binafsi naita ni uchafu, nasikitika sana kuona Jiji na Halmashari husika wameshindwa kabisa kudhibiti na kuwataftia eneo husika hii ni aibu"
Alizungumza mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambaye hupita mara kwa mara.
Picha na Dar es salaam yetu