Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all 16416 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBER 01, 2014

$
0
0

  




ENDELEA KUSOMA MAGAZETI MENGINE KWA KUBOFYA HAPA CHINI

















SHIRIKA LA TANESCO LISIKIKILIZE KILIO CHA WAKAZI WA MWANAGATI-KITUNDA

$
0
0
 Wananchi wa Mwanagati-Kitunda jijini Dar es Salaam  na maeneo jirani wamelilalamikia shirika la TANESCO  kwa kukatiwa umeme kwa siku tatu mfululizo, bila taarifa yoyote kutolewa kwa wakazi hao.''hatuna umeme kwa siku 3 mfululizo usiku na mchana mpaka sasa na hakuna taarifa zozote toka shirika la umeme Tanesco kuelezea hali hii inayoendelea mpaka sasa'',alilalama mmoja wa wakazi  wa eneo hilo.

Wakielezea kwa masikitiko makubwa juu ya tatizo hilo,Wananchi hao wamesema kuwa hawakupata taarifa yoyote ile toka Tanesco, na mpaka sasa wengi wao wamepata hasara kubwa kibiashara kutokana na tatizo hilo la kukosekana kwa umeme.

Mbali na matatizo hayo, Mji huo mpya ambao una chanzo chao cha kipekee kikubwa cha maji,kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kufanya wananchi hao kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi.

Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata sisi wakazi wa Managati-Kitunda



Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la umeme Tanesco ili kuelezea tatizo ili kwa wananchi wa Mwanagati - Kitunda zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii.

UTAFITI WAIBUA MAKUBWA NGONO ZA UTOTONI DAR

$
0
0
DSC_0140
Mratibu wa mradi wa PREPARE ambaye pia ni Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili, Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha SAMPULI tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono mwishoni mwa wiki kwenye kituo cha maelezo ya afya Muhimbili katika idara ya magonjwa ya akili. Kulia ni Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo.
DSC_0154
Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


DSC_0148
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo. Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Vicky Kimaro akiuliza swali kwenye mkutano huo.

Na Mwandishi wetu
SAMPULI tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono, imebainisha haja ya elimu ya afya ya uzazi kukabili hali ya sasa ya tabia hatarishi zinazowakabili vijana wadogo.
Matokeo ya awali ya mradi yalionesha kuwa asilimia 10 ya vijana wenye umri wa miaka 12 mpaka 14 ambao ni darasa la tano na sita waliofanyiwa utafiti walikuwa wameshawahi kufanya ngono na asilimia kubwa ikiwa ni kwa kutumia njia ya haja kubwa.
Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili,Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula.
“Vijana wengi walionekana wakifanya ngono ya uke na ya mdomo ikifuatiwa na ngono ya njia ya haja kubwa Kwa wale ambao wameshawahi kufanya ngono, asilimia 6.3 wamefanya ngono ya njia ya haja kubwa wakati asilimia 93.7 hawajawahi.”
Aidha alisema utumiaji wa kondomu ulionekana kuwa mdogo kwa vijana wadogo ambao wameanza kufanya ngono.
“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajawai kutumia kondomu kabisa wakati asilimia 32 wamewahi kutumia kondomu.”
Alisema utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa miaka minne ulioshirikisha Vyuo Vikuu vya Makerere cha Uganda, Cape Town na Limpopo vya Afrika Kusini, Bergen na Oslo vya Norway, Maastricht cha Uholanzi na Sussex cha nchini Uingereza.
Alisema utafiti umeonesha haja ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wadogo ambao bado hawajaanza ngono ili kuchelewesha kuanza ngono kwa mfumo wa kisaikolojia ili waweze kujitambua na kuacha kufuata nadharia za kisayansi pekee ambazo ndizo zinazotumika katika shule mbalimbali kuwaeleza mabadiliko ya miili yao.
Katika utekelezaji wa utafiti huo idadi ya wanafunzi 5,099 walichaguliwa mwanzoni mwa mradi kufanyiwa utafiti huo ambapo wanafunzi 4783 (asilimia 93.9) walifuatiliwa kwa miezi 6 na wengine 4370 (asilimia 85.8) walifuatiliwa kwa miezi 12.
Utafiti ulionesha elimu inayojishughulisha na masuala ya ujinsia na afya ya uzazi kwa vijana wadogo itumie mtazamo mpana utakaoleta mabadiliko ya msingi kwenye misingi ya virekebisho vya mabadiliko ya tabia.
Mradi huo wa PREPARE ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka manispaa ya Kinondoni zilizochaguliwa kwa kutumia taratibu sampuli mtawanyiko zilizopangwa katika makundi mawili ya shule za mwingilio yaani ilikotolewa elimu hiyo zilizokuwa 19 na za kulinganisha zilizokuwa 19.
Ili kuweza kupata matokeo yaliyokusudiwa mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watano wakufunzi wa wakufunzi; ulitoa mafunzo kwa walimu watekelezaji 76, na waelimishaji rika wanafunzi 132 na kuelekeza watoa huduma 8 wa afya katika kliniki za huduma rafiki kwa vijana ili kutekeleza muingiliano.
Tathmini iliyotoa majibu ya jinsi utendaji unavyoendelea na ya matokeo ilihusisha shule zote na wanafunzi zaidi ya 6,000 waliowekwa kwenye muingiliano, huku uchambuzi wa tathmini ukihusisha wanafunzi wenye umri wa miaka 12-14, wenye kujua kusoma na kuandika.
Matokeo yaliyotathminiwa ni Mabadiliko katika masuala ya ngono (kuanza ngono) na Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa wale waliokwisha anza ngono.
Kwa wastani mradi uliona kwamba mwingilio wa PREPARE ulipunguza uwezekano wa vijana wadogo (wavulana na wasichana) kuanza ngono na kuongeza uwezekanao wa kutumia kondomu kwa wale walioanza.
Hata hivyo, katika utekelezaji wa mradi mabadiliko katika uchukuaji wa hatua yalionekana zaidi miongoni mwa wasichana waliopata mwingilio ukilinganisha na wale ambao hawakupata mwingilio.
Uchukuaji wa hatua ulisababisha tabia ya kutumia kondomu miongoni mwa wanafunzi wa kiume lakini siyo miongoni mwa wanafunzi wa kike.
“Kimsingi tunataka kuwaambia wanahabari kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya mradi wa PREPARE ni kuchelewesha kuanza ngono miongoni mwa wanafunzi wa kiume na wa kike wenye umri wa miaka 12-14 katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania;
“Kuongeza uchukuaji wa hatua ulio chanya katika kutumia kondomu kwa jinsia zote na taarifa za ongezeko la utumiaji wa kondomu miongoni mwa vijana wa kiume. “
Mradi huu uliofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya, Programu ya utafiti wa afya umelenga kuangalia mwingilio ulio katika misingi ya utamaduni na jinsia, endelevu, kijamii ili kukuza ujinsia na afya ya uzazi miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 12-14 kwa kutumia shule kama njia ya kufundishia.

YAMOTO BAND YAFANYA MAKAMUZI YA NGUVU KWENYE CLUB YA MAISHA JIJINI DAR

$
0
0
 Yamoto Band wakiwa kwenye picha ya pamoja katika redcapert
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Temba akiwa na Yamoto bendi katika redcapert ndani ya club Maisha ya jijini Dar.
 Mkubwa na wanawe pamoja na Babu Tale wakiw kwenye picha ya pamoja kwenye shoo ya Yamoto Bandi iliyofanyika kwenye Club Maisha ya jijini Dar usiku wa kuamkia leo.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Aunt Ezekiel akiwa kwenye redcarpet alipokuja kushuhudua shoo ya Yamoto Band
  Full kujiachia ndani ya redcapert


 Ley Mond wa TIP TOP akitoa burudani kwa mashabiki wake waliofika kwenye ukumbi wa maisha jijini Dar.
 Dogo Janja akitoa burudani ya nguvu ndania ya Maisha Club ya jijini Dar alipowasindikiza Yamoto Bandi walipokuwa wanaitambulisha nyimbo yao mpya.
 Mc wa shoo D120 akiwaambia mashabiki wakae tayari kungalia Video ya nyimbo mpya ya band ya Yamoto uitwao "Niseme"
 Mashabiki wakiendelea kufuatilia kinachoendelea ndani ya Maisha Club kweye shoo ya Yamoto Band
 Said Fella (katikati) akiwa na vijana wake wa Mkubwa na wanawe alipokwa anatoa shukrani kwa wapenzi wa Yamoto Band waliofika kwenye uzinduzi wa nyimbo yao mpya iitwayo "NIseme"
 Yamoto Band wakiwaburudisha mashabiki wao kwenye Club ya Maisha ya Jijini Dar walipokuwa wanazindua Audio na Video ya nyimbo yao mpya iitwayo "Niseme"
 Mashabiki wakichukua kumbukumbu
Producer  wa Yamoto Band Shiriko mkubwa na wanae akiwapa burudani mashabiki waliofika kwenye club ya Maisha jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
 Dogo Aslay akimwimbia dada moja nyimbo zao kwenye uzinduzi wa nyimbo yao ndani ya Maisha Club ya jijini Dar
 Hapa ni furaha tu
 Dogo Aslay akiimba kwa hisia moja ya nyimbo za Yamoto Band
 Mmoja wa waimbaji wa Yamoto Band akitoa burudani ya nguvu kwenye ukumbi wa maisha jijini Dar nyuma ni madansa wao
  Mmoja wa waimbaji wa Yamoto Band akitoa burudani ya nguvu akipewa zawadi na mmoja wa mashabiki wao kwenye uzinduzi wa nyimbo yao mpya iitwayo "Niseme"
Hapa ni mwendo wa kucheza 



MRADI WA MAJARIBIO WA KUFUNDISHA MASOMO YA SAYANSI WA UNESCO WANEEMESHA TANZANIA

$
0
0
DSC_0018
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisoma risala ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za shirika hilo jijini Dar.
DSC_0015
DSC_0021  
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa juma.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


DSC_0009
DSC_0012
Na Mwandishi wetu
MRADI wa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na sayansi na utamaduni (UNESCO) na kuendeshwa na wizara ya elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 umemalizika kwa mafanikio huku wito ukitolewa kutafutwa njia ya kuendeleza mradi huo.
Tangu awali mradi huo haukuelezwa kinaga ubaga unakuaje endelevu kama utaonekana kuwa na manufaa kwa taifa.
Akitoa maelezo ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu,wataalamu na maofisa wa serikali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka wadau hao kuzingatia mafanikio yaliyokuwapo,kuangalia changamoto zake na kuona namna ya kuendeleza mazuri ya mradi.
Mradi huo wa majaribio ulifanyika katika shule za mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Morogoro, Kigoma na Tanga kwa upande wa Tanzania Bara.
Aidha ilielezwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Unesco kwa lengo la kuufunga rasmi pamoja na malengo yake ya kuboresha elimu Tanzania kwa kuhakikisha masomo ya sayansi yanafundishwa kwa namna inavyotakiwa, tathmini ilionesha udhaifu wa kutokuwepo na mpango madhubuti wa kuendelezwa kwake.

Mradi huu wa majaribio wa MSK ulilenga kukuza uwezo wa kufundisha masomo ya sayansi (baiolojia,kemia na fizikia) kwa shule ambazo hazina maabara kwakuzipatia visanduku vya majaribio pia uliendesha warsha mbalimbali ili kukuza uwezo wa matumizi ya zana zilizo katika mradi wa MSK pamoja na vitabu vya kufundishia.
Aidha mradi huo ulizingatia pia kuongeza upendo wa masomo ya sayansi kwa jamii na kuwafanya wanafunzi wapende na wawe na hamu na masomo ya sayansi.
Mradi huo ambao umefanyika kwa kuzingatia pia mahitaji ya taifa na kimataifa chini ya dhana ya kuendeleza masomo ya sayansi duniani unaendeshwa na UNESCO kwa kujenga uwezo wa shule za sekondari na msingi kufanya mazoezi ya utambuzi wa nadharia mbalimbali kimaabara hutoa masanduku maalumu ambayo yanakuwa ni kama maabara ndogo zinazotembea.
Maabara hizi hutoa uwezo wa kufanyika kwa majaribio ya msingi na yale makubwa kwa kuzingatia madaraja mbalimbali ya mafunzo kuanzia ngazi za chini kati na juu.
Katika ufungaji wa mradi huo uliofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti washiriki walielezwa maendeleo ya mradi hadi mwisho wake na changamoto zilizokuwa zinakabiliwa.
Unesco imesema kutanuka kwa kasi kwa elimu ya msingi kumesababisha changamoto za ubora wa elimu katika mfumo wa elimu nchini na mradi wa majaribio ulionesha kwamba ubora unaweza kurejeshwa kwa kuwa na mpango kama MSKs.

Kutokana na changamoto za raslimali kushindwa kuhakikisha kwamba kila darasa, mwalimu na mwanafunzi wanakuwa na zana zinazotakiwa kufundisha na kujifunza,walimu na wanafunzi walielemewa na hivyo kuathiri ufundishaji wa masomo ya sayansi ya baiolojia, kemia na fizikia.
Mathalani matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2011 wastani wa matokeo ya masomo ya sayansi kitaifa uliporomnoka chini ya asilimia 50.
Fizikia ilikuwa aislimia 43.2, kemia 43.3 na baiolojia 43.4 na katika takwimu hizo zilionesha kwamba wasichana walifanya vibaya zaidi.
Utafiti ulionesha wazi kwamba udhaifu huo umetokana na kukosekana kwa maabara, vifaa vya kufundishia na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi.
Pamoja na kuwepo kwa changamoto za uhaba wa masanduku haya ya maabara, tathmini iliyiofanywa ilionesha kwamba mradi ungeliweza kuunganishwa na miradi kama ya JICA na pia kutengenezewa mfumoi wa wa kuweza kuwa endelevu kutokana na umuhimu wake na ufanisi.
Changamoto kama za masanduku machache kuliko yalivyokusudiwa katika mradi , muda mfupi wa kufunza walimu na pia kutekeleza yote yaliyopangwa na suala la ukaguzi bado mradi huu kutokana na asili yake ungelikuwa na maana zaidi kuendelezwa ili kufikia zaidi shule zilizo pembezoni.

Aidha ili kuendelea na mradi huo tathmini iliyofanywa na kuelezwa na Ellen Binagi katika kikao cha wadau ilishauriwa serikali kufikiria kuanzisha vituo na taasisi za kutengeneza maabara hizo ndogo nchini badala ya kuagiza kutoka nje kutokana na gharama zake na hasa ikizingatiwa kwamba Tanzania ni nchi kubwa na yenye shule nyingi.
Binagi alisema kwamba kuanzishwa kwa mtindo huo kumeleta muonekano mpya katika upenzi wa masomo ya sayansi na katika shule za majaribio ufanisi wake ulikuwa mkubwa na ipo haja ya kuangalia namna ya kuendeleza.
Mtathmini huyo pia amesema ipo haja kwa UNESCO na serikali ya Tanzania pamoja na mradi kumalizika kuona namna ya kuuendeleza na kuondoa changamoto zilizoonekana wakati wa utekelezaji wake.

PONGEZI KWA JWTZ KWA KUTIMIZA MIAKA 50 TOKEA KUANZISHWA

$
0
0
 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye maonyesho Katika Uwanja wa Taifa.Picha na Maktaba.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa mazoezini.
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog. 
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo limetimiza Miaka 50 toka Kuanzishwa kwake mnamo tarehe 1/09/1964. JWTZ ni moja ya Jeshi lililotajwa na Mtandao mmoja hivi karibuni kuwa Ni Jeshi lenye weredi wa hali juu Duniani kutokana na Operesheni ambazo wamewahi kuzifanya na linalotumia Silaha za Kisasa. Baadhi ya Operesheni zilizowahi kufanywa na Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) ni Ile ya Kuwasambaratisha Waasi Wa M23 nchini Congo, Operesheni ya Comoro, Operesheni nyingine ni Ile ya Kulinda Amani Sudan wakiwa wameungana na Majeshi Mengine Kutoka Umoja wa Mataifa (UN)
Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) limejipatia Umaarufu na sifa kutokana na Kuwa na Askari wenye Nidhamu ya Hali ya Juu na Kuwachukulia Hatua kwa Haraka Askari wake ambao wameonyesha utovu wa Nidhamu kwa Wananchi na Jamii kwa Ujumla lakini Pia Sifa Hiyo Kubwa Imekuja Kutokana na uwezo mkubwa wa Kivita na Kuweza Kuwasambaratisha Waasi wa Kikundi cha M23 nchini Congo.
Jukumu kubwa la Kazi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Wavamizi na Vile vile Kushiriki katika kulinda Amani Katika Ngazi ya Kimataifa lakini Pia Pamoja na Majukumu hayo vilevile Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa Mstari wa Mbele katika Kujitoa kwenye shughuli za Kijamii kama Vile Matibabu, Elimu nk na Wamekuwa Mstari wa Mbele katika Kusaidia Jamii katika shughuli mbalimbali kama Vile za Uokoaji katika Maafa yanayotokea Nchini.
Kwa kifupi Sahivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa jeshi la Kisasa na wasomi ambao wanalisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii. Hongera ya Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa 

SOKA FESTIVAL MASSACHUSETTS CHINI YA UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NEW ENGLAND YAFANA

$
0
0
 Watanzania wa Massachusetts wakijumuika pamoja kwenye Soka Festival inayofanyika kila mwaka wakati wa majira ya joto.
Mkuu wa Wilaya ya Springfield Alhaji Isaac Kibodya katika picha ya pamoja na Gloria.
Manka na Jessica (kushoto) katika picha ya pamoja.
kwa picha zaidi bofya hapa

ELIHURUMA NGOWI JOINS SERENGETI BREWERIES LTD

$
0
0

Mr. Elihuruma Ngowi has joined Serengeti Breweries Ltd. as Brand Manager with a profound experience in Customer Care, Marketing and Sales after having spent over eight (8) years at Vodacom Tanzania Ltd.

At Vodacom, he worked in various departments from Customer Care to Marketing and finally with Sales & Distribution Department where he held key positions, most notably as Product Marketing Manager, Devices & Alternative Channels Manager and Franchise Operations Manager respectively. He is also the Vice President and co-founder of CIBN Tanzania Ltd.

Mr. Ngowi holds a Bachelor of Business Administration (Marketing) degree from the University of the Western Cape, Cape Town, South Africa. He also expects to graduate his master’s degree in International Business (Investment in Emerging markets) from the University of Dar es Salaam Business School later this year.

He is a strong believer on strong performance. He believes that one has to over deliver and outshines their performance. He also believes that people have to network with the right people, have a positive pride on your performance and be able to sell your results, successes and achievements and celebrate. Always treat people with high integrity and honesty and learn to hold courageous discussions. Spiritual powers should not be forgotten. Remember to say your prayers at all times.

DALILI TANO ZINAZOONYESHA ULICHAGUA TAALUMA ISIYOKUFAA

$
0
0

Umesikia watu wakisema“wanajifunza kutakana na makosa” ni kweli kwamba kila ufahamu tunaoupata unatokana na makosa tuliyokwisha kufanya wakati fulani. Lakini utasema nini pale ambapo unafanya taaluma ambayo umekosea? Je unafikiri utapata muda wa kujifunza kutakana na kosa hilo? Inawezekana hilo ni kosa litakalogharimu maisha yako kwa kiasi kikubwa.

Amini usiamini unaweza kubadilisha kazi mara tatu au mara nne kwa mwaka na hali yako ya kifedha isiathirike.
Kama umetumia miaka mitano kusoma kitu kisicho sahihi halafu unataka kubadilisha lazima uathirike kwa namna moja ama nyingine. Ni bora ujue toka mwanzoni kuhusu taaluma unayoiendea kabla ya kufanya makosa makubwa.
Kwa sasa inawezekana unafanya kazi na umechanganyikiwa, huyu mwandishi anamaanisha nini? Je hata mimi nimepotea? Hebu fuatilia maswali matano hapa ili uweze kujua kama uko kwenye taaluma sahihi au la!

Haufurahii kazi yako
Pale ambapo unaridhika na kazi unayofanya ndipo ni rahisi kujua umefanikiwa vile kwenye taaluma hiyo, lasivyo hautakuwa umefanikiwa. Kuna watu huamua kufuata taaluma fulani kwasabu watu wengine ameona wamefanikiwa, huo ni ujinga. Ingawa unahitaji kuchagua taaluma kulingana na ujuzi ulionao vilevile na utu /hulka na tabia ulizonazo. Usifuate mkumbo kwenye taaluma mwisho wake utaishia kuvunjika moyo na kupata msongo wa mawazo.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Utendaji wako wa kazi hauendi Vizuri
Kitu kingine ambacho kinaonyesha uko katika taaluma sahihi ni utendaji wako wa kazi. Utendaji wako wa kazi unaokuwa vizuri na haukupi shida inawezekana kwa kiasi kikubwa uko mahala sahihi, hivyo bila kufanya juhudi hauwezi kwenda hatua ya juu. Ingawa kuna mashirika mengine hupandisha vyeo watu waliokaa muds mrefu kazini kitu ambacho sio sahihi. Kama utendaji wako wa kazi unashuka kila mara, inawezekana hauko sehemu sahihi hivyo fanya maamuzi ya msingi hapo.

Hujaridhika na Majukumu yako ya kazi
Hata kama umepandishwa cheo lakini majukumu ya kazi yako huyapendi au hujaridhika nayo inamaanisha uko kwenye taaluma ambayo si ya kwako. Kumbuka kuridhika na kazi pamoja na majukumu take ni kitu cha msingi kinachokusaidia kufanikiwa na kukujenga kitaaluma na ndipo utakapoonyesha umefanikiwa.

Una Msongo wa Mawazo au Kutojielewa
Msongo wa mawazo na kutojielewa ni vitu ambavyo huwapata sana watu ambao wanafanya kazi. Ingawa kazi ambayo inakupa msiongo wa mawazo mwingi inaathiri afya yako pole pole na inaweza kukusababishia kushindwa kufanya kazi wakati mwingine. Kama Msongo wa mawazo ni kitu kisichokoma kwenye taaluma uliyopo chukua tahadhari umepotea njia.

Unafikiria kuacha kazi na kurudi shule
Hili ni kosa kubwa ambalo wafanyakazi wengi hulifanya. Wengi huacha kazi kwa sababu hawawezi kusoma na kufanya kazi wakati mmoja, hiyo ni njia mbaya au maamuzi mabaya kama unataka kufanya taaluma sahihi. Kwa mtu kama huyu mfumo wa elimu umebadilika na sio kama zamani, siku hizi kuna vyuo vinatoa elimu kupitia njia ya mtandao.
Kwahiyo unahitaji kuchukua fursa ya mtandao na wakati huo huo unaendelea kupata uzoefu katika kazi unayofanya. Na vile vile elimu kwa njia ya mtandao ni kitu ambacho wengi wanaweza kufanya kwa sababu ya gharama kuwa chini ni urahisi wa kuendelea kusoma. Unapofuata hatua hizi hautapata shida dana ya kujua taaluma sahihi unayotaka kuichukua, kazi kwako. Unaruhusiwa kutoa mchango wako na namna ulivyopata taaluma sahihi kwa ajili yako.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO AZINDUA VIKOBA MKOANI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey Zambi akifafanua jambo wakati alipokuwa alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa vicoba mkoani Dodoma uliofanyika katika viwanja vya Nyerere.
 Mlezi wa Vicoba mkoani Dodoma Anthon Mavunde akipeana mikono na Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey Zambi wakati wa uzinduzi wa Vicoba uliofanyika juzi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Wanachama wa kikundi cha vicoba cha kilimani a' wakishangilia mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili baada ya kujiwekea hisa za shilingi 23 mili na kupata zawadi ya laki tano toka makao makuu ya vicoba nchini.
 Mmoja wa wanavicoba akikabidhiwa friji ya kampuni ya cocacola baada ya kufuzu vigezo vya biashara ya vinywaji na Naibu waziri huyo.
 Rais wa Vicoba Nchini Devota Likokola akiiwa na baazi ya viongozi waliokuwa meza kuu wakati wa uzinduzi huo.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBER 2, 2014

$
0
0






ENDELEA KUSOMA MAGAZETI MENGINE KWA KUBOFYA HAPA CHINI






























RAIS KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA DODOMA-FUFU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiraia ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km70.9) huku akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA, Ndugu Kuniaki Amatsu kulia huku Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km 70.9) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe pamoja na viongozi wengine.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Taaswira ya mkeka mpya kutoka Dodoma hadi Fufu wa Kilomita 70.9 aliouzindua Rais Kikwete
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakimtazama Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA Ndugu Kuniaki Amatsu na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania bi Tonia Kandiero walipokuwa wakipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Fufu(Kilomita 70.9)
 Waziri wa zamani wa Ujenzi Mzee Job Lusinde akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi wa rasmi wa barabara ya Iringa-Dodoma sehemu ya Dodoma-Fufu (Kilomita 70.9) huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge wakishuhudia tukio hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli  pamoja na viongozi wengine wakitaifa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma-Iringa sehemu ya Dodoma- Fufu Kilomita 70.9. Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini –Wizara ya Ujenzi

UTAFITI: HIZI NDIZO DALILI ZINAZOONESHA KWAMBA MPENZI WAKO AMEANZA MAHUSIANO NA MTU MWINGINE

$
0
0

Mwaka 2012 ulifanyika utafiti Uliogundua kwamba asilimia 30 mpaka 50 (30%-50%) ya wanawake wangekubali kuwa na mwanaume mwingine endapo tu watathibitishiwa kwa asilimia mia moja (100%) kwamba wapenzi wao hawatajua! Utafiti ambao haukufanikiwa kwa upande wa wanaume ambao wengi wao hawakutaka kuwa wakweli! Ukweli ni kwamba hakuna kinacholeta aman moyoni kama uhusiano usio na udanganyifu!

Lakini suala linaloulizwa na watu wengi ni je, ntajuajuaje mpenzi wangu ananidanganya?  Usihofu Tumekuandalia ishara hizi muhimu kujua mpenzi wako anakudanganya.

ONYO: Usimuhukumu mtu kwa ishara moja tu na kufanya hitimisho kuwa ameanza mahusiano na mpenzi mwingine. Kumbuka dalili hizi kila moja ni onyo tu na tumia zaidi ya moja kugundua kama anakudanganya.

DALILI ZA WANAWAKE WADANGANYIFU
1.Anakuwa mkali kujibu maswali rahisi, Wakati mwingine hukuuliza kwanza wewe kabla ya kukujibu!
 Kisaikolojia hii huonesha ni akili ya kutaka kusema uongo. Mfano; umetoka wapi usiku huu? Jibu: kwan nini unaniuliza swali kama hilo? Au hujui kama leo ni birthday ya janet? Au pengine kwanini unanifuatilia siku hizi? Hiyo ni taa nyekundu.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


2. Umuhimu wako anapungua kwake, Hujali zaidi Muonekano wake kuliko zamani, na hutumia muda mwingi kujiremba hasa anapotoka peke yake!
  Utagundua vile vitu alivyozoea kukuomba, kukuuliza, na kukushirikisha havipo tena. Unafikiri havipo tena? Hapana!  Vipo ila kuna mtu mwingine anayeulizwa au kushirikishwa kwenye masuala hayo. Inawezekana alikuwa akirudi nyumbani anakusimulia siku yake ilivyokuwa, changamoto nk lakini sasa ukimuuliza  siku yako iliendaje hugeukia pembeni na kujibu kwa jibu moja tu “nzuri” na kutumia muda wake mwingi kujiremba.

3.Kuna Rafiki mpya kajitokeza na Siku hizi na hataki tena kuwa karibu na ndugu/ rafiki zako
Mara chache anaweza kukutambulisha kwa rafiki huyu mpya, anaweza kusema ni mfanyakazi mwenzangu, mwanafunzi mwenzangu, au hata ni rafiki yangu tulipotezana muda mrefu!
 Cha ajabu ni kwamba, hupenda kumlinda na kusimama upande wake na kuwa mkali unapotaka kujua zaidi kuhusu rafiki huyu mgeni. Hatotaka pia ujue anakaa wapi, jina lake halisi nk!

4.Hapendi ujue ratiba yake, anataka ajue yako! Hataki umsindikize tena, anataka aende na rafiki zake! Neon “sisi” hubadilika na kuwa “mimi”
Hupendelea zaidi kukuuliza ratiba yako na kutokupa nafasi ya kuingilia ratiba yake. Hufanya hivi ili kujua atakuwa huru kiasi gani kufanya mambo yake. Na sehemu alipopenda kuweka neon sisi hubadilika na kuwa mbinafsi zaidi “mimi”. Hii hutokea hata anapozungumzia mambo yajayo.

5. Simu yake imekuwa kitu cha siri, na  huweka password (Haikuwa tabia yake)
Unapoona mpenzi wako kaanza kuwa mkali unapotaka kugusa simu yake, au hutoa sababu ya haraka akikuta tu umeshika simu yake (mfano hebu nipe mara moja nimpigie mama) hii sio dalili nzuri. Pia akitoka huchukua muda mrefu kupokea simu au kuacha ikate ndo akupigie, hii inawezekana anatafuta sehemu nzuri akae ndipo apokee simu hiyo ili usijue yuko wapi! Wakati mwingine hutoka na kwenda kuongelea mbali mnapokuwa pamoja, au hata kuacha simu nyumbani mnapotoka.

DALILI ZA WANAUME WADANGANYIFU

1.Haachi Simu yake muda wowote
Umeacha kuiona simu yake mezani akiwa hayupo? Kuna muda anaweza kuingia nayo mpka bafuni! Hutoa sababu kama “nasoma sana habari kutumia simu yangu” au kuna taarifa muhimu nataka kufuatilia siwezi acha simu yangu,hutoa sababu ya haraka akikuta tu umeshika simu yake (mfano hebu nipe mara moja nimpigie bosi nilikuta missed call yake) hii sio dalili nzuri.

2.Huwa Msiri na hataki ujue mambo yake huwa mkali sana unapoonesha kuumdadisi
Moja Ya Silaha za wanaume ni Kukutishia pale anapoona unaingia sana kwenye maisha yake binafsi. Huwa mkali sana unapomuuliza kuwa alikuwa wapi au kujua ratiba zake.

3.Kuna Rafiki mpya kajitokeza na pengine kutajwa mara kadhaa
Mara chache anaweza kukutambulisha kwa rafiki huyu mpya, anaweza kusema ni mfanyakazi mwenzangu, mwanafunzi mwenzangu, au hata ni rafiki yangu tulipotezana muda mrefu. Cha ajabu ni kwamba, hupenda kumlinda na kusimama upande wake na kuwa mkali unapotaka kujua zaidi kuhusu rafiki huyu mgeni. Hatotaka pia ujue anakaa wapi, jina lake halisi nk!

4.Safari zinaongezeka, na hataki muwe pamoja
Mpenzi wako kaongeza safari, pengine za kwenda mji  jirani kila weekend, au hataki kufuatana na wewe kama zamani, Hataki umsindikize stendi/airport au bandarini (pengine alikokuaga anaende sio anakokwenda) Huja amechoka na hataki kuwa karibu na wewe.

5.Anakutuhumu sana kwamba una mpenzi mwingine (Iwapo tu huna mpenzi mwingine)
Hii ni njia nyingine wanaume huitumia kujihami pale anapoona unaweza kumhisi anauhusiano na mpenzi mwingine. Hii humfanya mwanamke aogope kuzungumzia suala la udanganyifu kwenye uhusiano wao kwani akizungumzia tu, kibao kitageuka na kuanza kutuhumiwa yeye.

USHAURI
Hata hivyo, binadamu tunatofautiana hivyo usimuhukumu mtu kwa kuona ishara moja tu ambayo inaweza kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kimaisha kama, maisha magumu, kazi, shule, magonjwa nk. Cha muhimu ni kuhakikisha  unatimiza wajibu wako kwa asilimia mia moja (100%) kwani pengine hii ndio sababu ya yeye kuwa na mpenzi wa nje. Pia ni jukumu lenu wote wawili kuonyesha. BAKI NJIA KUU MICHEPUO SIO DILI

NA  KUMI MUHIMU

KAMPUNI YA UJERUMANI YAELEZEA KIINI CHA VURUGU KWENYE SHOW YA DIAMOND, YAAHIDI SHOW YA BURE KUWAPOZA MASHABIKI

$
0
0
 Kampuni ya Britts Event iliyohusika kuandaa show ya Diamond Stuttgart, Ujerumani imeeleza kwa kina kiini cha vurugu kubwa zilizotokea kwenye show hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa huku baadhi ya watu wakijeruhiwa vibaya.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Awin Williams Akpomiemie ameeleza kwa kina kuhusu mzozo uliokuwepo ndani ya kampuni hiyo ulioathiri show hiyo kwa ujumla.
Hiki ndicho alichokisema:
Watu wangu awali ya yote, ningependa kuelezea moyo wangu kwa kuuambia umma na mashabiki wa Diamond Platnumz, kwamba sisi kutoka uongozi wa Britts Events tunaomba radhi kwa kile kilichotokea usiku uliopita, wakati wa show ya Diamond Platnumz. Haikuwa imepangwa show ichelewe kuanza au kwa msanii kutotumbuiza. 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hapa ntawaeleza ukweli wote wa kile kilichotokea katika tamasha hilo kwakuwa ninyi nyote mnataka kuujua ukweli.
Mradi wa Diamond ulikuwa wa gharama kubwa sana kwakuwa uongozi Britts Events ulitaka kila kitu kiwe  professional. Kama kampuni tuliamua kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye mradi huu hivyo tuliwafuata wawekezaji watatu lakini mmoja wao hakuwekeza sana kwani alidai hatokuwa nchini.
Wawekezaji wawili ni watu wanaofahamika sana jijini Stuttgart, mmoja anafanya kazi na jeshi la Marekani na mwingine anamiliki kampuni ya usafirishaji mjini Stuttgart. Hawa ndio wawekezaji wakubwa tuliowapata. Tuliwapa mikataba wasaini lakini yule mwenye kampuni ya usafirishaji alikataa kusaini mkataba wa mradi huo kwakuwa alitaka kuwa na mkataba wake binafsi na yule jamaa wa Marekani. Kisha nilimwambia Mr.USA kuwa hiyo haikuwa hatua sahihi lakini  Mr.USA  alisema ‘Britts msiwe na shaka, kila kitu kitakuwa poa.
Watu wangu, mradi ulianza na kisha wale wawekezaji wawili wakagundua kuwa Diamond ni msanii mkubwa na angevuta umati mkubwa wa watu na watu wanampenda. Kisha walijiunga pamoja dhidi ya Britts waliowaalika kama wawekezaji kwenye mradi huo na walitaka kuuchukua kutoka kwa Britts sababu ni wao ndio walioleta sehemu ya fedha kwaajili ya mradi huu wakati Britts ndio wanaommiliki msanii na mradi wenyewe. Ila tu kwakuwa Britts ni kampuni mpya mjini Stuttgart, Mr. Shipping Guy aliamua kuungana na yule jamaa wa Marekani na DJ Wanted, kuuchukua mradi.
Pindi Britts ilipokaa chini na kufanya mkutano nao, walikuwa wakifanya mkutano wao wenyewe na kubadilisha mipango yote hivyo walikuwa wanahujumu na kuendelea na mradi nyuma ya Britts. Britts ina makubaliano nao kuwa pindi msanii atakapowasili Ujerumani, watampa balance ya 3.250 euros, na walikubaliana na kigezo hicho kwasababu Diamond aliweka wazi kuwa bila fedha asingepanda ndege.
Waliniomba mimi niongee na Diamond kuwa watampa fedha kwenye uwanja wa ndege, lakini unajua nini? Kabla Diamond hajawasili Mr. USA na Mr. Shipping Guy pamoja na DJ Wanted walitaka kuandaa wahuni kumuiba msanii kutoka kwenye show ya Britts lakini Britts walikuwa wajanja na walimchukua msanii kabla hawajafanya chochote. Hapo ndipo shida ilipoanzia.
Huko Essen kabla Britts haijafika huko, USA Guy na Shipping Guy, walikuwa wameshapeleka wafanyakazi wapya kuchukua show na kuwafukuza wafanyakazi wa mwanzo. Kisha Britts ilikuwa ikilumbana nao kuwa wao ni wawekezaji tu na sio waratibu wa kampuni, kwanini wanataka kuhodhi tukio kwasababu mnataka kutengeneza fedha na sio kujali watu. Britts baadaye ilikuja kugundua kuwa wafanyakazi waliowapeleka walikuwa wapenzi wao wa zamani na ndugu zao.
Dhumuni la kufanya hivyo lilikuwa ni kuiba fedha na kutofuata mkataba na Britts, hivyo baada ya Diamond kuwasili Stuttgart usiku wa saa tano, alikuwa amechoka lakini wawekezaji hawakujali. Walikuwa wakifirikia tu jinsi wanavyoweza kurudisha fedha zao. Diamond alisema anahitaji fedha yake lakini Shipping Guy na USA Guy walikataa kumpa fedha Diamond wakihisi kuwa Britts wanataka fedha ya ziada.
Kisha usiku ulipoingia sana, waliweza kutoa 3.000 euros na ilikuwa saa tisa na nusu tayari lakini Diamond aliendelea kukataa kutumbuiza kwakuwa alidai ni lazima wamlipe fedha iliyosalia ambayo ni 250 euros, kitu ambacho ni haki yake kutokana na makubaliano.

 Mpaka muda Mr Shipping Guy na Mr USA Guy wanagundua kuwa Britts walikuwa wakifanya kitu sahihi kwa kuwaomba walipe fedha hizo kwa Diamond, tulikuwa tumeshachelewa na watu walikuwa wameshaanza kupigana wakati huo Diamond alikuwa ndani ya gari mbele tu ya ukumbi, na kama ningemruhusu atoke wangemuua.
Tunavyoongea hapa, Mr USA anadai kuwa fedha tulizoingiza kwenye tukio zima ziliibwa na watu hivyo Britts Events haiwezi kupata fedha kutoka kwenye tukio tuliloliandaa na kulimiliki. Hiyo ilikuwa mipango yao kuchukua biashara ya mtu mwingine kutokana na tama.
Britts Events inawapenda, Britts Events ilitaka kila mtu awe na furaha,  Britts Event haijawahi kuahidi msanii yeyote na asije. Na niamini hata tulipofanya show ya Bracket tulikuwa na kitu kile kile kutoka kwa wawekezaji. Walipoona kuwa show inaweza kuwa na mafanikio walitaka kupewa asilimia 50% ya kampuni.
Well, sitakiwi kusema yote haya kwakuwa ni jambo la uongozi lakini niliamua kuweka mambo sawa, siwezi kuficha tena. Tuna Waafrika wengi wenye tamaa wanaotaka kuchukua biashara za watu wengine sababu ya tamaa. Lengo letu ni kuwafanya muwe na furaha na sio kupoteza muda na fedha zenu. Tunafahamu kuwa nyote mlitoka sehemu za mbali, mliacha watoto wenu na familia.
Uongozi wa Britts Events unaomba radhi kwa hili. Hivyo msiilamu Britts Events lakini laumuni tamaa za Mr. USA Guy na Mr. Shipping Guy.  Tunawapenda na tunaahidi show ya bure ya Diamond hivi karibuni.

Credit: Bongo5

PICHA: HARUSI YAFANYIKA NDANI YA MAJI NCHINI CHINA

$
0
0
 Katika mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.
 Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii. 
 Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
'Mtindo tofauti wa picha'
''Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.n"maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ''
 Hawa ni wateja wake, Lin Enxiao na He Huan.
Ndoa yao haijawa tayari kwani wataoana mwaka ujao, lakini wapenzi wengi wachina wanasema wameamua kujipiga picha zao za harusi mapema ili wasipate tatizo lolote. ''Marafiki wetu wengi walijipiga picha katika eneo kavu,'' asema YY. "sisi tulitaka kitu tofauti. ''
Watu wanapofikiria kuhusu picha za harusi, wao hutaka kujipiga sehemu kavu kuliko kuta nyeupe au nyasi, '' asema Lamea. "sisi tunahisi vyema kubadili mtindo huo.''
Tina Liu mmiliki wa duka la Mr Wedding
Sio mara ya kwanza kuona watu wakipigwa picha wakiwa ndani ya maji wala China sio nchi ya kwanza kuanzisha mtindo huu, ila China imeanza kuitumia kwa njia ambayo imewapendeza wengi.
'Vipodozi visivyoharibiwa na maji'
Kuna studio nyingi za picha zinazotoa huduma hii nchini China, soko lina ushindani mkali lakini baadhi ya wafanyabiashara hawana maadili ya kazi.
''Baadhi ya wafanyabiashara wana uelewa wa kazi na ni wabunifu lakini huwa hawadumu kwa sababu wanakosa maadili ya kazi. ''
Duka hili la Mr Wedding lina wabunifu wengi ambao huwa wanawapendekezea maharusi namna ya kupigia picha , wakitumia muda mwingi kuwapodoa na kuwapamba nywele maharusi.
"tunapendekeza bibi harusi akiwa ndani ya maji avalie gauni nyeupe na ndefu. Na sisi hutumia vipodozi ambavyo haviwezi kuharibiwa na maji. ''
Kisha maharusi hawa wanatembezwa na kuingizwa ndani ya tenki ya maji ambako wanapigiwa picha.
Tenki hiyo huwa na maji ya vuguvugu na mtu wa kuwasidia maharusi pia huwa ndani ya tenki hiyo ambamo wanapigiwa picha.
Tina alianza kazi hii mwaka 2003 wakati huo akipiga picha tu za kawaida za harusi kabla ya kuanza kuwapiga picha watu wakiwa ndani ya maji.
Kila biashara zina changamoto zake. Kwa Tina lazima awe na maarifa ya utenda kazi ili kazi yake iweze kunawiri.

CHANZO: BBC SWAHILI

MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA ENEO LA UBUNGO MAJI JIJINI DAR

$
0
0
 Wasamalia wema wakijaribu kuokoa maisha ya dada aliyegongwa na gari (daladala) maeneo ya Ubungo maji wakati akivuka barabara. 
Mwanamke mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande wa Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster lililodaiwa kuvunja sheria likiwa  linapita kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi. Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali. 
Mwili wa dada huyo akichukuliwa kwenye gari na wasamaria wema baada ya kukutwa umaiti.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


HiIi ndilo gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T454 BBV lililomgonga dada huyo.
Mmoja wa mashuda wa ajali ameiambia blog hii ya Pamoja kuwa mama huyo alipogongwa na daladala lá inayofanya kazi zake kutoka Mbezi - Muhimbili alafu likamburuza yapata mita kumi na tano, baada ya daladala kusimama yule mama akawa anajitahidi kutoka pale uvunguni  lakini ilishindikana na damu zilikuwa zinavuja kichwani. Mpaka walipo shuka abiiria wote waliokuwa wamepanda daladala hiyo na kuliinua na kumtoa mama huyo kwenye daladala ,na baada ya kutokea ajali hiyo dereva wa daladala hiyo alikimbia. Na mwanamke huyo amefariki papo hapo maana alitokwa damu nyingi kichwani na mwili wake umepelekwa  hospitali ya Muhimbili.

AFISA FEKI WA USALAMA WA TAIFA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonesha waandishi wa habari silaha zilizokamatwa na jeshi ilo 
Silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI




MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBER 03, 2014

$
0
0






ENDELEA KUSOMA MAGAZETI MENGINE KWA KUBOFYA HAPA CHINI





















AYSHA CHEYO NDIYE MISS TANZANIA USA PAGEANT 2014

$
0
0
Miss Tanzania USA Pageant wa 2013 Joy Kalemera akimvisha taji miss Tanzania USA pageant 2014 Aysha Cheyo siku ya Jumamosi Aug 31, 2014 Baada ya kunyakua taji hilo kwenye mashindano ya umiss yaliyofanyika Slvr Spring, Maryland nchini Marekani.
Miss Tanzania USA pageant 2013 Joy Kalemera akipigia makofi mshindi mpya wa taji hilo Aysha Cheyo mara tu baada ya kumaliza kumvika taji hilo.


ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Mshindi wa taji la miss Tanzania USA Pageant Aysha Cheyo akiwa na furaha ya kunyakua taji hilo.
Aysha Cheyo na Joy Kalemera wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey.
Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Aysha Cheyo akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Kupewa Mushala (kushoto) na mshindi wa tatu Jessica Lavius na miss Congeniality ni Grace Mlingi.

PICHA: MWANDISHI MWINGINE 'ACHINJWA' NA KIKUNDI CHA ISIS

$
0
0

 Mwandishi aliyechinjwa na ISIS Steven Sotloff.
Wapiganaji wa dola ya Kiislam ISIS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia wa Marekani Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji hao. Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwakajana.
Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley. Wapiganaji hao katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza.
Mfuafi wa ISIS akishika kisu alichotumia kumchinjia Steven Sotloff.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutomuua mtoto wake. Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest amesema kuwa maofisa wa Marekani wanaendelea na uchunguzi wa ripoti hiyo.
Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya ISIS nchini Iraq. Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya wapiganaji wa ISIS ni kulipa kisasi kwa Marekani.

Viewing all 16416 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>