Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all 16416 articles
Browse latest View live

CRISTIANO RONALDO AWA MCHEZAJI BORA ULAYA

$
0
0
 Mchezaji nyota wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akibusu tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kukabidhiwa usiku wa kuamkia leo mjini Monaco, Ufaransa.
 Cristiano Ronaldo akifurahia.
Wachezaji wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer (kushoto) na winga Mholanzi Arjen Robben (kulia) pamoja na Ronaldo (katikati) akifurahia baada ya kushinda tuzo hiyo.

YALIYOJIRI KATIKA SHOO YA TWANGA PEPETA KWENYE CLUB YA MAISHA JIJINI DAR

$
0
0
  Kiongozi na mwimbaji  wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu (katikati) akiimba pamoja na waimbaji wake kwenye shoo iliyofanyika kwenye club ya maisha jijini Dar

 Mwimbaji wa Twanga Pepeta, Salehe Kupaza akiimba kwa hisia kubwa kwa mashabiki wao waliofika kutizama shoo yao ya nguvu kulia ni  Kiongozi na mwimbaji  wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


  Haji Ramadhani(wa kwanza kulia) akiimba pamoja na waimbaji wenzake wa Twanga Pepeta kwenye club ya Maisha jijini Dar
 Mwimbaji wa Twanga Pepeta, Kalala Junior (aliyeshika mike) akiendelea kuwaburudisha mashabiki wao kwenye ukumbi wa maisha jijini Dar


Wacheza shoo wa Twanga Pepeta wakifanya ya kwao kwenye club ya Maisha jijini Dar.

ZITTO: SINA UHUSIANO NA MWASITI WALA DIVA

$
0
0


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kukana kuwa na mahusiano na mtangazaji wa Clouds FM, Loveness ‘Diva’ pamoja na msanii wa muziki, Mwasiti.
Zitto alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi cha EATV ambapo alikanusha kuwa na uhusiano wowote wa mapenzi na mastaa hao licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na Diva.

“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.
Katika hatua nyingine Zitto alizungumzia pia tetesi kuwa ana uhusiano mwingine na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote.
“Naumia sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.
Aidha, mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mchumba wake aliyemtaja kwa jina moja la Jack na wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.

Source:GPL

HAKIKISHA UNAWEZA KUJIBU MASWALI HAYA KABLA YA KWENDA KWENYE USAILI (INTERVIEW)

$
0
0
1.Tuelezee kuhusu wewe kwa ujumla (tell us about yourself)

2.Mipango gani umejiwekea kwenye maisha yako? Na umefanya nini kuitimiza?

3. Kwanini Tukuajiri wewe na sio mtu mwingine? (waelezee uwezo wako).

4 Kwa nini unaitaka nafasi/kazi hii? Na kwa nini unaacha nafasi/kazi uliyokuwa nayo?
 (usianze kumkandia mwajiri wako aliyepita kama uliajiriwa)

5 Ni Kipindi gani kigumu ulichowahi kukumbana nacho, na ulifanya nini kukikabili?

6. Tueleze Uwezo na udhaifu wako

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

7. Unapenda Kufanya kazi katika mazingira ya aina gani?

8. Unafanyaje kukabiliana na “Stress” na kufanya kazi kwa shinikizo?

9 Unaifahamu vipi kampuni yetu?

10. Ni makosa gani Umeshawahi kuyafanya na  unayajutia kwa kiasi fulan? (mtego)

NB: Kumbuka unaweza pia kupewa nafasi ya kuuliza swali lolote hivyo ni vema na wewe ukajiandaa kwa hilo.

NA KUMI MUHIMU


UPDATES:WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI LEO.

$
0
0
Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 

Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea 
 Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
 Ilikuwa ni Ajali mbaya 

Mashuhuda 
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya 

WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
 Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
 Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
 Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
 Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
NA MBEYA YETU BLOG

JWTZ LATOA MSAADA KWA WAZEE NA MAYATIMA ZANZIBAR

$
0
0
WANAJESHI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishusha msaada wa vyakula na vifaa vya kufanyia usafi vilivyotolewa na jeshi hilo kwa Wazee wanaoishi katika nyumba za Wazee ziliopo Welezo Wilaya ya Magharib.Kushoto anaeshughudia Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi na Kaimu Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Kanali Shaban Ilangu Lissu.
KAIMU Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Kanali Shaban Ilangu Lissu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi msaada wa vyakula na vifaa vya kufanyia usafi vilivyotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)kwa Wazee wanaoishi katika nyumba za Wazee Sebleni ikiwa ni kutimiza miaka 50 ya kuanzishwa kwa JWTZ.Kulia Naibu Katibu Mkuu Uwezeshaji na Ushirika, Nd. Ali Khamis.



ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

MKUU wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akiwakabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya kufanyia usafi Watoto yatima wanaoishi katika nyumba za mayatima Mazizini. Msaada huo ulitolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya kuanzishwa kwake.




























MKUU wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akizungumza na Wazee wanaoishi katika nyumba za Wazee Sebleni mjini Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya usafi vilivyotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya jeshi hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964.
WAZEE wanaoishi katika nyumba za wazee Sebleni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi (hayupo pichani) wakati akizungumza katika makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya jeshi hilo.
MASISTA wanaowalea wazee wanaoishi katika nyumba za wazee welezo wakiwa katika hafla ya kumakabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya Jeshi hilo ambapo misaada kama hiyo ilitolewa kwa Tanzania nzima kwa wazee wasiojiweza na mayatima.
MKUU wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika nyumba za mazizini, baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula vilivyotolewa na JWTZ katika kutimiza miaka 50 ya jeshi hilo.(Picha na Haroub Hussein).

MPYAA: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KUTOKA TANROADS

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AUGUST 30, 2014

$
0
0






ENDELEA KUSOMA MAGAZETI MENGINE KWA KUBOFYA HAPA CHINI


























MISS TANZANIA USA PAGEANT YAPAMBA MOTO, MAMISS WAANZA KUWASILI TAYARI KUWASHA MOTO LEO JUMAMOSI

$
0
0

 Miss Tanzania USA Pageant leo inafikia ukingoni itakapofanyika Downtown, Silver Spring Maryland nchini Marekani katika picha Jesca Kalemera (aliyesimama) akijinoa mwishomwisho mbele ya washiriki wenzake huku Pendo Rancy (kushoto) mmoja ya waratibu wa Miss Tanzania USA Pageant akimsikiliza wengine katika picha ni washiriki wa Miss Tanzania USA Pageant 2014 Maria Rutayuga (wapili toka kushoto), Mercy Sukaya (watatu toka kushoto) ambaye anatokea Michigan na anayefuatia ni Grace Mlingi.
 Washiriki wa Miss Tanzania USA Pageant wakifuatilia jambo kutoka kushoto ni Maria Rutayuga, Mercy Sukaya na Grace Mlingi.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Kushoto ni Pendo Rancy mmoja ya waratibu akimsikiliza mmoja ya washiriki wa Miss Tanzania USA Pageant (hayupo pichani) huku Maria Rutayuga akifuatilia kwa makini.
 Pendo Rancy akiwaeleza jambo washiriki wa miss Tanzania Usa Pageant walipokua wakijinoa mwisho mwisho kwa ajili ya Jumamosi Aug 30, 2014 watakapo washa moto kumtafuta miss Tanzania USA Pageant mpya.
 Kutoka kushoto ni Maria Rutayuga kuotoka Maryland, Jesca Kalemera kutoka New Jersey, Mercy Sukaya kutoka Michigan na Grace Mlingi kutaoka Maryland.
 Washiriki wakimsikiliza mmoja ya waratibu alipokua akiwaelekeza jambo kwenye hotel waliyofikia ya Double Tree iliyopo Dwntown Silver Spring.


RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA DARAJA LA GULWE MPWAPWA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu pamoja na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene, akiweka jiwe la msingi kama ishara ya kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170 litakalo unganisha kati ya Wilaya ya Mpwapwa na Kibakwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania Jacob Chimeleja, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu, Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe,  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya  pamoja na Mkandarasi,viongozi wa dini na kitaifa mara baada ya Rais kuzindua rasmi ujenzi wa daraja la Gulwe.
 Daraja la Gulwe linalotumika sasa kama linavyoonekana hali iliyopelekea Serikali ya awamu ya nne kupitia Wizara ya Ujenzi kuanza kujenga daraja kubwa na la kisasa la Gulwe litakalokuwa na mita 170 mara baada ya kukamilika kwake.

 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akipita mbele ya Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa Mita 170.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi ERB Profesa Ninatubu Lema watatu kutoka kulia pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakifatilia ngoma za asili kabla ya uzinduzi rasmi wa Daraja la Gulwe
 Ujenzi wa Makalvati yatakayosaidia Daraja kupitisha maji katika mto Gulwe kama yanavyoonekana. Jumla ya Makalvati tisa yatajengwa katika daraja hilo la mita 170.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ili kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na Mbunge wa zamani wa Mpwapwa George Malima Lubeleje kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia akiwatambulisha Wakurugenzi, Wenyeviti, Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Gulwe litakalokuwa na mita 170.
=====  ========

Jiwe la msingi daraja la Gulwe-Wilayani Mpwapwa.

Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kuwa ujenzi wa daraja la Gulwe katika mto Sinyasungwi ni mwanzo wa ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa-Kibakwe yenye urefu wa kilomita 101, kwa kiwango cha lami.

Akiweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 170 na uwezo wa kupitisha tani 150 rais kikwete amesema daraja hilo licha ya kuunganisha jimbo la Mpwapwa na Kibakwe pia litamaliza kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiathiri barabara na reli katika eneo la Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa.

“Kukamilika kwa daraja hili itakuwa jawabu la kudumu kwa reli na barabara katika eneo la Gulwe na hivyo kazi yenu sasa ni kutunza mazingira ili maji yafuate mkondo na hivyo kutoathiri miundombinu na mashamba ili kukuza shughuli za kilimo”,amesisitiza Rais Kikwete.

Naye Waziri wa ujenzi Dkt. John Magufuli amezungumzia umuhimu wa halmashauri nchini ikiwemo ya Mpwapwa kutumia fedha za mfuko wa barabara kujenga barabara zake kwa kiwango cha lami ili kuboresha miundombinu ya miji na kuwataka wananchi kuacha kuchimba mchanga karibu na madaraja na barabara ili kulinda miundombinu hiyo na kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu.

Dkt. Magufuli amesema ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa-Kibakwe hadi Chipogoro yenye urefu wa kilomita 120, utafanyika kwa awamu tatu ambazo ni Mbande-Kongwa-Mpwapwa, Mpwapwa-Kibakwe na Kibakwe-Chipogoro ili kuiunganisha barabara hiyo na ile ya tanzam na hivyo kuiunganisha wilaya ya Mpwapwa na kupunguza magari yaendayo Morogoro na Dare s salaam kupitia Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS), mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170 utahusisha ujenzi wa makalvati 9 yatakayosaidiana na daraja kupitisha maji na barabara ya kilomita 1.5 kila upande wa daraja na linatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.3 litakapokamilika na litakuwa na uwezo wa kubeba tani 150 kwa wakati mmoja.

UTAFITI: HIVI NDIVYO VYAKULA VYA KUONGEZA KINGA YA MWILI

$
0
0


Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni yakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako.

1.Yogurt (yogati):
Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako.

2 Matunda:
Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, matunda asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda .

3. Vitunguu saumu:
Hupatikana Kila soko Tanzania. Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Vitumie kwa kutafuna (kama unaweza) au weka kwenye chakula.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
4. Uyoga:
 Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

5. Supu ya kuku:
Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto  husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla.

6.Viazi vitamu (mbatata)
Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba  ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.

7.Karoti
Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi.

8. Samaki
Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

9. Matikiti
Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.

RASIMU YA WARIOBA SASA MIFUPA MITUPU

$
0
0
Kamati za Bunge Maalumu, zimekamilisha kazi ya kujadili na kuchambua Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, huku ikiwa imefanyiwa mabadiliko makubwa tofauti na ilivyokuwa awali.
Wajumbe wanatarajiwa kuanza kukutana kama Bunge zima kuanzia Jumanne ijayo, Septemba 2, 2014 wakati kamati zitakaposoma taarifa zake baada ya kufanya uchambuzi wa sura 15 za Rasimu ya Katiba kwa zaidi ya wiki tatu, huku yakitarajiwa mabadiliko makubwa.
Mabadiliko yaliyofanywa yameondoa mambo makubwa yaliyokuwa yakiifanya rasimu hiyo kuonekana mpya, hivyo sasa baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaiona rasimu kama ‘Katiba ya 1977 iliyofanyiwa marekebisho.’
Mwelekeo wa kubadili karibu misingi yote muhimu iliyojengwa na tume iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba akiwa mwenyekiti, ilianza baada ya kuwekwa kando kwa mfumo wa muungano wa Serikali tatu uliopendekezwa na badala yake kurejea katika muundo wa sasa wa serikali mbili.
ENDELEA  KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Uamuzi huo uliathiri mtiririko na muundo mzima wa sura na ibara za rasimu hiyo, kwani sasa wajumbe wa Bunge Maalumu walilazimika kutengeneza Katiba yenye mwelekeo wa serikali mbili na siyo tatu tena zilizokuwa zimependekezwa na tume.
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba mwelekeo wa uchambuzi wa rasimu kwa sura hizo 15, lazima ufuate kile ambacho kamati zilikiamua katika uchambuzi wa awali wa sura ya kwanza na ya sita.
Miongoni mwa mambo ambayo yameachwa baada ya kurejesha mfumo wa serikali mbili ni muundo wa uongozi wa juu wa nchi hususan nafasi ya Makamu wa Rais, muundo wa Bunge la Jamhuri, kupunguzwa mamlaka ya Rais, uwajibikaji na uwajibishwaji wa wabunge na ukomo wa ubunge.
Kadhalika, habari kutoka ndani ya kamati zilisema suala la kuwekwa kwa maadili ya uongozi kwenye Katiba nalo lilizua mjadala mkali kutokana na baadhi ya wajumbe kutaka liondolewe kwa maelezo kwamba linapaswa litajwe kwenye sheria na siyo Katiba.
Mambo ya muungano
Miongoni mwa mambo ambayo kuna kila dalili kwamba yatabadilika ni Bunge Maalumu kuongeza mambo ya muungano kutoka saba yaliyopendekezwa na tume na huenda idadi yake ikazidi 22 yaliyomo kwenye Katiba ya sasa.
 Uchunguzi wa gazeti hili uliofanywa katika baadhi ya kamati za Bunge hilo na kuthibitishwa na baadhi ya wenyeviti wake, umebaini kuwa yapo mapendekezo ya mambo ya muungano kuongezwa, tofauti na mtazamo wa awali kwamba yangepungua kama moja ya njia za kuondoa kero za muungano.
Tume ya Jaji Warioba ilipendekeza mambo saba tu kwenye orodha ya muungano chini ya mfumo wa Serikali tatu, mfumo ambao hata hivyo ni dhahiri umeshawekwa kando na Bunge Maalumu na kurejesha muundo wa serikali mbili.
Mambo yaliyopendekezwa na tume hiyo ambayo yapo kwenye sura ya 17 ya Rasimu ya Katiba inayohusu masharti ya mpito ni pamoja na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uraia na Uhamiaji.
 Mengine ni Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje, Usajili wa Vyama vya Siasa na Ushuru wa Bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
 Mapendekezo hayo yaliyaacha nje mambo mengine 15 yaliyopo kwenye Katiba ya sasa ambayo ni polisi, mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, mikopo na biashara ya nchi za nje, utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu na leseni ya viwanda na takwimu.
Pia yamo elimu ya juu, maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa na gesi asilia, Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania, usafiri na usafirishaji wa anga, utafiti, utafiti wa hali ya hewa na  Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
 Baadhi ya wenyeviti wa kamati za Bunge Maalumu wamesema kuna kila dalili kwamba baadhi ya mambo yaliyoachwa yatarejeshwa huku kukiwa na mtazamo kwamba mengine yanaweza kuongezwa kutoka nje ya orodha ya sasa.
 Mwenyekiti wa Kamati Namba Tano, Hamad Rashid Mohamed alisema orodha iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba ina upungufu mkubwa kwani imeacha mambo mengi ya msingi yenye sura ya muungano.
“Mathalani huwezi kuzungumzia kwamba usalama ni suala la muungano halafu ukaacha mambo ya anga, au ukaacha suala la mitihani, yaani Baraza la Mitihani limeachwa pia suala la utafiti nalo huwezi kuliacha, kwa hiyo orodha itaongezeka,” alisema Mohamed.
Mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita, Stephen Wassira alisema kuna mambo mengi ya muungano yaliyotajwa kwenye Rasimu ya Katiba lakini hayako katika orodha iliyowekwa kama moja ya nyongeza kwenye rasimu hiyo.
“Ngoja nikwambie kwamba mambo hayo yataongezeka, hilo halina ubishi na kamati yangu tulijadili kidogo na kesho (leo) tutakutana kumalizia. Ukisoma vizuri ibara kwa ibara, utagundua kuwa kuna mambo mengi kama vile Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo ni chombo cha muungano hata ukiangalia muundo wake,” alisema Wassira.
Alitaja mambo mengine kuwa mahakama ya juu inayopendekezwa kuanzishwa lakini haimo kwenye orodha pamoja na masuala ya elimu ya juu na utafiti.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati Namba nne, Christopher Ole Sendeka alisema kuna kazi kubwa ya kutazama upya orodha ya mambo ya muungano na kwamba suala la usalama wa anga ni moja ya mambo hayo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati Namba Moja, Ummy Mwalimu alisema, licha ya kwamba kamati yake haikujadili suala hilo lakini orodha hiyo inaweza kuongezeka kwani kuna mambo mengi yameachwa.
“Leo tulikuwa tunaangalia suala la fedha na kuna mambo ukichuguza humo yanagusa sehemu zote mbili, sisi hatukujadili sehemu hiyo kutokana na kwamba haikuwa kwenye orodha ya kazi tulizopewa ila nadhani tukipata fursa bungeni lazina mambo hayo yaangaliwe,” alisema Mwalimu.
Kamati nyingine ambayo haikujadili suala hilo ni namba tatu ambayo mwenyekiti wake, Dk Francis Michael alisema orodha ya mambo ya muungano iko kwenye sura ya 17 ambayo haikuwa sehemu ya kazi za kamati.
CHAZO: MWANANCHI

AJALI: WATU WATATU WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI KUINGIA MTARONI ENEO LA KIJITONYAMA, JIJINI DAR

$
0
0
 Mchina aliyekuwamo kwenye gari akizungumza kwa simu, pembeni yake ni askari wa usalama barabarani.
Watu watatu akiwemo raia wa China na dereva ambaye ni mtanzania wamenusurika kufa katika ajali iliyotokea maeneo ya Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikihusisha gari ndogo aina ya Opa.
 Dereva wa Opa ambaye hakufahamika jina lake mara moja.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la zimamoto lililokuwa linatokea njia ya Mikocheni kuingia barabara kubwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Watu wakishuhudia gari likitolewa mtaroni.
“Gari la fire lilikuwa kasi sana huku likipiga king’ora, kwa hiyo kujihami dereva mwenye Opa akajikuta ameingia mtaroni, tunashukuru hakuna aliyeumia,’’ alisema Robert.



Aidha mtu mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo ni Abdukarim ambaye alikuwa ndani ya mtaro huo akisafisha. Askari wa usalama barabarani alifika eneo la tukio huku break down likianza kuitoa gari hiyo mtaroni.
 Gari la break down likivuta Opa iliyoingia mtaroni.
Aliyenusurika katika ajali hiyo, Abdukarim akiwa pembeni akitafakali.

NI LEO FAINALI YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) NDANI YA MLIMANI CITY

$
0
0

SOUTHERN AFRICAN FASHION SHOW YAFANYIKA KWA KISHINDO

$
0
0
Washereheshaji wakifanya vitu vyao kwenye usiku wa onesho la mavazi kutoka kwa wanamitindo na wabunifu mbalimbali kutoka nchi kusini mwa Afrika wakiwemo wabunifu wawili Watanzania waliopendezesha maonesho hayo.
 
Juu na chini ni bendera kutoka nchini za kusini mwa Afrika zikipita kwenye ufunguzi wa maonesho hayo yaliyofanyika siku ya Ijumaa Aug 29, 2014 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


kwa picha zaidi bofya hapa

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AUGUST 31, 2014

$
0
0







MWANAAFA MWINZAGO AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 NA KUONDOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA KITANZANIA

$
0
0
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza akitoa neno kwa wadau waliojitokeza kushuhudia fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililokuwa pia likirushwa live kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya Watanzania.
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni Jana Katika Ukumbi wa Mlimani City.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Washiriki wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 waliofanikiwa kuingia Kumi Bora wakiwa wanasubiri mshindi atangazwe 
Host Wa TMT 2014 Joti akimpongeza Baba wa Mwanaafa Mwizago kwa Mwanae kuibuka Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) na kuibuka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Mwanaafa Akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 na kuibuka na kitita cha Shilingi milioni 50.
Lulu akionyesha Bahasha iliyokuwa na JIna la Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) ambae ni Mwanaafa Mwinzago na Kumfanya kujishindia Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia fainali ya TMT ambayo ilikua ikirushwa live kupitia ITV.
Malaika Band wakitoa Burudani wakati wa fainali ya TMT 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo.
Christian Bella Akitoa burudani kwa kuimba wimbo wa Nani kama Mama ambao uliamsha Shamra Shamra katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo na Mwanaafa Mwinzago Kuibuka Mshindi.
Majaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 
Joti akitoa Suprize ya ukweli haswa katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Proin Promotions, Geofrey Lukaza akiwa na Mkewe katika Red Carpet Kabla ya Show Kuanza katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo
 Mc Pilipili Akifanya Yake
 Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions Limited wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya MShindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) kupatikana na kila Mmoja kusherehekea Ushindi huo

TAHADHALI: UPEPO MKALI UNAOAMBATANA NA MAWIMBI MAKUBWA VINATARAJIWA KATIKA MAENEO YOTE YA UKANDA WA PWANI

$
0
0



MKOA WA KAGERA WACHUKUA TAHADHARI DHIDI YA EBOLA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akitoa ufafanuzi namna Serikali livyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola mkoani humo kwa kuongeza vifaa kinga na kuwawezesha kielimu wataalam wa afya wanaofanya kazi ya uchunguzi wa dalili za ugonjwa huo walioko katika vituo vya ukaguzi mpakani.
Afisa Afya wa Kituo cha ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi Bw. Amos Mangaluke akipitia fomu zilizojazwa na raia kutoka nje ya nchi wanaotumia mpaka huo kufuatia zoezi la uchunguzi wa dalili za awali za ugonjwa wa Ebola linalofanyika kituoni hapo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Ofisi ya Uhamiaji ya Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi.
Kizuizi cha magari katika mpaka wa Kabanga unaotenganisha Tanzania na Burundi, Wilayani Ngara.


Na. Aron Msigwa –MAELEZO,Kagera.

Mkoa wa Kagera umechukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa kuongeza nguvu katika udhibiti na ukaguzi wa raia wa kigeni kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaoingia nchini Tanzania kupitia vituo vya mpakani vya mkoa huo.

Akizungumza katika mahojiano maalum wilayani Ngara, Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe amesema kuwa kufuatia hali hiyo serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeongeza vifaa kinga na kuwawezesha kielimu wataalam wa afya walioko katika hospitali za mkoa huo na vituo vya ukaguzi mpakani.

Amesema kuwa mkoa huo kijiografia unapakana na nchi tatu zikiwemo Uganda kwa upande wa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi na kuongeza kuwa mkoa kupitia kamati za Afya na wataalam wa afya walioko maeneo yote ya vituo vya ukaguzi wanafanya kazi zao ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa kila anayeingia nchini kupitia vituo hivyo anachunguzwa dalili za Ebola.

“Mkoa wa Kagera kama tunavyojua unapakana kwa karibu sana na nchi za Burundi, Rwanda na Uganda, kuna mwingiliano mkubwa sana wa watu kutoka eneo moja kwenda jingine hapa lazima tuchukue tahadhari kubwa , ninawahakikishia wananchi kuwa tumejipanga vizuri katika kuimarisha uchunguzi kupitia kamati zetu za afya” Amesisitiza.

Amesema kufuatia uwepo wa ugonjwa huo katika nchi ya jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uongozi wa mkoa kupitia kamati ya Afya na ile ya Ulinzi na Usalama unaendelea kuwaelimisha wananchi kupitia vituo vya mbalimbali vya radio vya mkoa huo kuhusu dalili za ugonjwa huo , namna ya kujikinga na namna ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo watabaini mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.

Kwa upande wake Afisa Afya wa Kituo cha ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi Bw. Amos Mangaluke akizungumzia hali ya ukaguzi wa raia wanaoingia nchini kupitia mpaka huo amesema kuwa zoezi la uchunguzi wa dalili za awali za ugonjwa wa Ebola linafanyika kwa ufanisi mkubwa kufuatia kituo chake kuwa na vifaa kinga vinavyomsaidia wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema takribani watu 500 wanaotumia mpaka huo wa Kabanga huchunguzwa afya zao kwa siku ambapo hujaza fomu maalum ya taarifa ambayo hutumiwa na wataalam wa afya kituoni hapo.

DIAMOND PLATNUMZ AOKOLEWA NA POLISI WA UJERUMANI KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA.

$
0
0
 Hii ndio hali halisi ya ukumbi ulioharibiwa na washabiki mjini Stuttgart, nchini Ujerumani
Polisi wakimuokoa Diamond na kama si polisi Diamond sijui ingekuwaje

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show, washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake.
 Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa. Moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake  na mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptalini, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatalini. 
 Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria, ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart mengi kuhusu Diamondo na hii ni moja wapo ya Source yetu STUTTGARTER NACHRICHTEN DE
Viewing all 16416 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>