Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

AJALI YATOKEA MWANDEGE IKIHUSISHA TOYOTA HIACE NA LORI LA MAFUTA MKOANI PWANI

$
0
0
Watu wanne wapo katika hali mbaya na wengine saba wamejeruhiwa baada ya lori scania namba T653 BFD  (scania 380) kugongana uso kwa uso na basi dogo la abiria Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda mkuranga.
Abiria wawili waloikuwa mbele  ya daladala walikatika miguu.Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo iliyotokea Mwandege, Dominic Kubhota, ameiambia blogu hii kwamba chanzo cha ajali hiyo ni ovateki isiyotumia akili ya lori hilo .Majeruhi hao wamefikishwa katika hospitali ya Mkuranga, lakini muda mfupi baadaye walianza kukimbizwa kuleta Dar es salaam kwamatibabu zaidi.
Majeruhi wengine walioweza kuzungumza ni:
1. Mustafa mfungapoa wa mkuranga
2. Abdul Ally wa mwandege
3. Ramadhani rajab
4. Theofrida Mwinuka ( alikuwa mbele amevunjika miguu)
5. Jamal  mbaraka ( aliyekwanguka ngozi ya kichwa)
6. Abraham Mohamed
7. Swalehe salum
NA LUKWANGULE 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>