Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiongea na wanahabari .
Waziri Membe akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Pembeni ni watu alioambatana nao.
Waziri Membe akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Pembeni ni watu alioambatana nao.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
WAZIRI wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Kamilius Membe amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya jambo la msingi kuwaita na kuwaonya makada wake (akiwemo yeye) wanaotuhumiwa kukivuruga chama kwa kuendesha kampeni za kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwakani kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mh. Membe alisema haoni kibaya kilichofanywa na CCM hivyo ataheshimu maamuzi yaliyotolewa huku akisisitiza kuwa ni lazima kiongozi ajulikane kwa wananchi mapema.
“Kama chama kitashindwa kukemea mienendo mibaya ya wanachama, wake, basi hakifai kuwepo, hivyo jambo lililofanywa na Chama Cha Mapinduzi ni sahihi, kuliko kuacha watu wanaojiita wameoteshwa kuendelea kukivuruga,” alisema Membe
Mbali na sula hilo, Mh. Membe alisema Tanzania imeingia katika uwakilishi wa Baraza la Usalama na Amani la Afrika, pia itapeleka majeshi ya kulinda amani nchini Sudan Kusini.
Aidha, alizungumzia suala la mgogoro wa mpaka baina ya nchi mbili za Tanzania na Malawi ambapo amesema nchi hizo zitaitwa na jopo la wasuluhishi wakiwemo wanasheria wa kimataifa ili kuona kipi ni sahihi juu ya mgogoro huo.
Pia, Mh. Membe amegusia vita ya maneno baina ya Tanzania na Rwanda ambapo ameweka wazi kuwa hakuna uhasama baina ya nchi hizo mbili kama inavyokuzwa na vyombo vya habari huku akiitaka nchi ya Rwanda kutoifikiria vibaya Tanzania inapokuwa karibu na wapinzani wake.
“Kwa hiyo hakuna uhasama mkubwa kati yetu na Rwanda, wale ni majirani zetu, hivyo mambo yasikuzwe zaidi ya uhalisia,” alisema Membe.
CHANZO: GPL