Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

FACEBOOK YANUNUA APPLICATION YA 'WHATSAPP' KWA DOLA BILIONI 19

$
0
0

Facebook wanazidi kujitanua zaidi kibiashara katika ulimwengu huu wa dijiti ambapo wameweza kufanya makubalino na waanzilishi wa ‘WhatsApp’, Jan Koum na Brian Acton kuinunua kwa makubaliano ya jumla ya dola bilioni 19 pamoja na hisa.

Mwanzilisihi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa walianza kuzungumzia hatua hiyo siku 11 zilizopita ili waweze kuimiliki WhatsApp ambayo hivi sasa inawatumiaji zaidi ya milioni 450 kwa mwezi.

Mwanzilishi wa WhatsApp ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya Yahoo!, Jan Koum ameonesha kulifurahia deal hilo na kudai kuwa ni heshima kwao kwa kuwa mbali na pesa watakazolipwa, yeye pia atakuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Facebook.

“We’re excited and honoured to patner with Mark and Facebook as we continue to bring our product to more people around the world.” Alisema Jan Koum.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Ingawa mmiliki wa Facebook anaamini kwamba kwa kutumia WhatsApp wataweza kuwavuta mabilioni ya watumiaji, amesisitiza kuwa hana mpango wa kuweka matangazo kwenye mfumo huo na kwamba hadhani kama kuweka matangazo kwenye mfumo wa kutuma ujumbe ni njia bora zaidi ya kutengeneza pesa.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Facebook italipa fedha taslim dola bilioni 4 na kiasi cha hisa zake kinachokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 12, na ziada ya dola bilioni 3 zitakazolipwa baadae.

Deal hilo litakapokamili na wakalipwa kiasi hicho, waanzilishi wa WhatsApp Jan Koum na Brian Acton wanatarajiwa kutangazwa kuwa mabilionea wapya.

Kampni ya WhatsApp Inc. ilianzishwa mwaka 2009 na watu wawili waliokuwa wafanyakazi wa kampni ya Yahoo, mmarekani Brian Aton na raia wa Ukrain Jan Koum, ambapo wanadai kuwa kwa hivi sasa huwasajili watumiaji wapya milioni moja kwa siku.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>