Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI AWASILI MKOANI RUKWA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

$
0
0


Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima akishuka kwenye ndege aina ya Auric Air katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mapema jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Rukwa kufuatia mwaliko wa Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akimtambulisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga jana.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akisalimiana na mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Chrissant Mzindakaya katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na msafara wa Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima ofisini kwake jana. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kukubali mwaliko wake. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameahidi kuboresha miundombinu ya viteule vya jeshi vilivyopo Mkoani Rukwa ukiwepo usafiri, majengo na nishati ya umeme wa jua.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akisalimiana na rafiki yake wa siku nyingi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luten Kanali Sipe mara baada baada ya kuonana na msafara wa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ofisini kwake jana.  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>