Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

SOMA HAPA ALICHOSEMA WAZIRI WA UINGEREZA KUHUSU UJANGILI NCHINI

$
0
0
 Ujangili nchini Tanzania unavyoshika kasi. Picha na Maktaba 
Tunakabiliwa na janga. Faru wanauawa na maharamia kila baada ya dakika 10 na ni wachache kuliko chui 3,500 ambao wamebaki porini.
Hili siyo tatizo tu la kimazingira. Kwa tembo 25,000 kuuawa mwaka 2011 na 22,000 kuuawa mwaka 2012, ni ishara inayoonyesha kuwa biashara haramu ya wanyama pori sasa imekuwa ni uhalifu wa kidunia wenye nguvu ya kuathiri maendeleo ya kiuchumi, kusababisha migogoro, kuimarisha vikundi vya kigaidi na kuathiri watu wenye hali duni ya watu waishio katika umaskini.
Ujangili unaathiri jamii barani Afrika, hususan yale maeneo katika bara ambapo wanakabiliwa na hali mbaya ya janga la ujangili. Kuna kazi muhimu inaendelea kila siku katika bara zima kushughulikia; kuanzisha jitihada za uhifadhi nchini Namibia au uzoefu wa kiteknolojia mpya nchini Kenya.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kazi hii imekuwa na athari mbaya kwani zaidi ya askari wa wanyamapori 1000 wamekwisha uawa ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita. Afrika inaongoza katika mwitikio wa kisiasa kwa hatua zilizochukuliwa katika Mkutano wa Afrika juu ya tembo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana (2013) sambamba na jitihada za Gabon katika kuliibua hili katika Umoja wa Mataifa.
Uongozi ulioonyeshwa na Botswana, Gabon na nchi nyingine ndivyo haswa inavyohitajika kulikabili na kulimaliza tatizo.
Lakini ujangili na biashara haramu ya wanyamapori ni suala linaloigusa dunia nzima. Biashara haramu ya wanyamapori ni mtandao wa kutisha wa kiuhalifu ambao una thamani ya mabilioni na ina fursa ya kuyumbisha ukanda na kutishia ustawi wa kimaendeleo endelevu.
Hatupaswi kuiachia Afrika ikabiliane na tatizo hili bila kuwasaidia. Lazima wote tuonje madhara ya uhalifu wa wanyamapori kuanzia usafishaji wa fedha haramu hadi kuharibu mazingira.
Ni jukumu letu kusaidia uongozi ambao nchi za Kiafrika na kwingineno wanaonyesha juu ya suala hili. Hivi karibuni, tumeridhia Mpango Kazi katika Serikali namna ya kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori.
Pia tumetangaza ruzuku mpya za thamani ya paundi milioni 10 kwa miradi ambayo inalenga kukabiliana na ujangili wa tembo na biashara nyingine haramu za wanyamapori na tutatoa taarifa kwa kina baada ya kufahamu mfumo tutakaotumia kutoa ruzuku hizi.
Mnamo Februari 13, Uingereza ilikaribisha Serikali mbalimbali za Afrika, Asia, Amerika na Ulaya kuleta juhudi za pamoja za kimataifa.
Tanzania ilikuwa nchi yenye uwakilishi wa kipekee kwa kuwakilishwa na Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. Hili ni jambo lililoleta hamasa na kuonyesha dhamira imara na umakini wa Tanzania katika kushughulikia tatizo la ujangili.
Waziri Nyalandu mnamo Februari 8 mwaka huu (2014) alisema; “Ukizingatia uzito wa tatizo la ujangili linaloikabili Tanzania, Serikali imedhamiria kupambana na kuushinda ujangili”.
Msisitizo wa Mkutano wa London ulikuwa ni katika kuboresha na kuimarisha sheria, kumudu kukamata na kuwachukulia hatua wale wanaohusika na ujangili na biashara haramu; kusaidia jitihada za kuimarisha na kuboresha mazingira endelevu kwa maeneo yale ambayo yanaathirika na uhalifu unaofanywa kwa wanyamapori na kupunguza uhitaji wa bidhaa zitokanazo na wanyamapori kwani kwa uhitaji wa bidhaa hizo ndipo inakuwa kichocheo cha biashara hizo.
Tunatumaini Serikali mbalimbali katika mkutano wa Uingereza umeondoka na kauli moja ya kuungana nasi katika kuweka azma ya juu ya kisiasa katika kushughulikia uhalifu wa wanyamapori na kutusaidia hasa mataifa yanayoathirika na suala hili katika kupambana dhidi yake. Hatuwezi kuendelea kusubiri kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumechelewa sana kuokoa uwepo wa aina hii za kipekee za viumbe.
Na endapo kwa umoja wetu hatutaweza kuwalinda, basi tutakabiliwa na tatizo kubwa sana la kuweza kulinda hata jamii nyingine ya viumbe ambavyo havijulikani sana dhidi ya uharamia huu.
Akizungumza katika mkutano wa wahisani wa kukabiliana na uharamia wa kusafirisha wanyamapori Februari 3 ulioandaliwa na Waziri Nyalandu, Balozi wa Uingereza Dianna Melrose alitoa dukuduku lake juu ya ukuaji wa ujangili:
“Uhalifu wa wanyamapori hasa ujangili dhidi ya tembo nchini Tanzania hakika upo katika kiwango cha hali tete ya kuwa janga.
Ripoti ya hivi karibuni juu ya Takwimu za Tembo kwa mbuga za Selous-Mikumi na Ruaha-Rungwa inaonyesha idadi ya tembo katika maeneo haya kwa sasa ipo 13,084 na 20,090.
Hii ni anguko la kitakwimu kwa kiasi cha mbili ya tatu toka mwaka 2009. Mbuga ya Selous ni hifadhi ya kidunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO). Inabidi zichukuliwe hatua za haraka za kukomesha mauaji haya hatari dhidi ya tembo wa Tanzania.
Lakini Tanzania na nchi zingine haziwezi kutekeleza jukumu hili peke yao. Ni jukumu letu sote. Jitihada pana zenye kuhusisha njia zote zinapaswa kutumika hasa kuzilenga nchi ambazo ndizo vyanzo; nchi za kusafirisha sambamba na nchi hitaji.
Ni matumaini yangu makubwa Serikali za nchi zitakazohudhuria Mkutano wa London baadae mwezi huu zitaonyesha azma ya hali ya juu ya kisiasa kushughulikia uhalifu dhidi ya wanyamapori na kusaidia nchi kama Tanzania katika mapambano haya. Hatuwezi kuchelewa zaidi”.
Mark Simmonds ni Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Masuala ya Bara la Afrika.
 MWANANCHI

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>