Na Abdulaziz Ahmeid,Kilwa Masoko
Familia moja ya Bw Bernad Towele dereva wa Gari la Takukuru Wilayani Kilwa Imenusurika baada ya Nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia katika mji mdogo wa kilwa masoko.
Akithibitisha kutokea kwa tukio la Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 6 usiku kuamkia leo,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,Joseph Mfungomara alieleza kuwa chanzo cha Moto huo bado hakijajulikana ila hakuna majeruhi.
Kamanda Mfungomara alimalizia kuwa Vitu vyote vilivyomo katika nyumba hiyo vyenye thamani ya Tshs 7,700,000/ Havikuweza kuokolewa.
Baadhi ya Wananchi waliopo katika mji huo Akiwemo Mfanya biashara Ahmaid Shukra na Saidi Timamy mmiliki wa kituo cha Mafuta cha Alsat wameiomba Halmashauri hiyo kupeleka ombi maalum serikalini ili waletewe gari la Zimamoto kutokana na wilaya hiyo kuanza uwekezaji unaotokana na Raslimali ya Gesi ya Songosongo pamoja kukua kwa mji huo mashuhuri Afrika ya Mashariki