Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAMBO YA KUANGALIA UNAPOKUWA NA MARAFIKI WA KAZINI

$
0
0


Katika mazingira yoyote ya kazi, watu wana marafiki ambao huhisi kuwa zaidi ya mtu “unayefanya nae kazi tu” mahusiano haya ya kazini husaidia kazi kufanyika, lakini kuna mambo ambayo yanatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa unapokuwa na marafiki wa kazini;
  • Kama shule ya msingi, ofisini kuna watu wakorofi, waongo, wenye hasira kali, wanafiki, wambea, wavivu. Kwa bahati mbaya mambo ya namna hiyo hayaishi kiwepesi .

  • Kama umejikuta ofisini umeangukia kundi la watu ambalo hujitenga na wafanyakazi wengine, wasengenyaji, wenye kufuatilia maisha ya watu jiondoe kwenye kundi hilo. Kama shule kuna mtu atakuja kuliondoa kundi hilo, hivyo angalia usijeondoka nalo. .
  • Jaribu kuwa rafiki wa kila mtu, hata kwa wale ambao hawako karibu na wewe. Huwezi amini jinsi watu wanavyowapenda watu ambao ni wacheshi na ni marafiki wa kila mtu, itasaidia wakati unauhitaji au tatizo watu wengine wakusaidie.
  • Kitu cha muhimu na ushauri unatakiwa kuwafahamu vizuri marafiki zako wa kazini wakoje. Kwa kila kitu kinachoendelea ofisini, siasa zake, siri, tumaini, ndoto usijeukaruhusu mtu asiye rafiki wa kweli kukugeuka au kukusaliti na kuharibu mwelekeo wa taaluma yako. Hatua ya kwanza fahamu hulka za rafiki wa kazini na tabia zao kabla ya kuanza kuwashirikisha na kuongea vitu vingi kuhusu wewe.
  • Kwa wafanyakazi wote, marafiki au sio marafiki , fanya utani kwa umakini wakati wote uonekane kikazi.
Nenda kwenye matukio ya kiofisi, fanya utani unaohusiana na kazi, kula na kufurahi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>