Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group, ambayo inamiliki Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Robert Kisena (wa pili kishoto), akipokea mfano wa funguo ya gari, kuashiria kupokea mabasi 175 aina ya Eicher, kutoka kwa Rais wa Kampuni ya Eicher ya India, Anurag Vohra, wakati wa hafla fupi ya kuikabidhi mabasi hayo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mabasi hayo 175 yanafanya idadi ya mabasi 280 kati ya 1000 yalinunuliwa na kampuni hiyo yanayofanya safari zake jijini Dar es Salaam. (Picha na Joseph Senga)
↧