Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakipata vinywaji wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali na Kampuni ya Msama Promotions.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mwandaliwa Islamic Orphans, Halima Mpeta (kushoto), akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka katika mfuko wa tamasha la Pasaka, kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotins, Alex Msama.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi mtotio, Heid Din, kwa niaba ya watoto wenzake sehemu ya msaada wa vyakula uliotokana na mfuko wa tamasha la Krismasi wenye thamani ya sh. Milioni 4, kupitia mfuko wa tamasha la Pasaka kampuni hiyo imetoa sh. Milioni 2.5. Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni Kituo cha Malaika cha Mwananyamala, Kituo cha Mwandaliwa Islamic Orphans cha Mbweni na Kituo cha Tovichido cha Temeke. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi kiasi cha sh. laki 7 mlezi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Tovichido, Honoratha Michaele kwa ajili ya kulipia ada za shule za watoto hao.
Watoto wanaoishi katika kituo cha Malaika cha Mwananyamala wakipokea hundi ya sh. laki 7 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kwa ajili ya kusaidia ada za watotoi wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo baada ya kukabidhi misaada kwa vituo vitatu vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions waandaaji wa Matamasha ya Kirimasi na Pasaka jana ilikabidhi misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya jijini Dar es Salaam, ikitimiza ahadi ya kuisaidia jamii kabla ya Tamasha la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama misaada hiyo iliyogharimu shilingi milioni 7 imekabidhiwa katika vituo vya TUVUCHIDO cha Temeke Maganga, Malaika Kids cha Mwananyamala na kituo cha Yatima cha Mwandaliwa.
Msama alisema katika sehemu ya msaada huo pesa taslim shilingi milioni 2.9 ni ada kwa wanafunzi na nyingine ni kwa vifaa mbalimbali yakiwemo madaftari, sabuni za mche, unga, mafuta ya kupaka na sukari.
Aidha Msama alisema misaada hiyo imetokana na mfuko wa Tamasha la Pasaka kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Krismasi ambalo walikabidhi misaada ya shilingi milioni 4.
Mkurugenzi wa TOVICHIDO, Honarata Michael alimpongeza Msama kwa kuwajali watoto na jamii kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa, Halima Mpeta alisema anamshukuru Msama kwa kujali jamii kwani katika kituo chake si mara ya kwanza kukisaidia na amezidi kumuomba aendelee na moyo wa kukisaidia kituo chake na vingene vyenye mahitaji.