Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MTU MMOJA AKUTWA AMEJINYONGA KWENYE UFUKWE WA SPICE HOTEL MJINI BUKOBA

$
0
0
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Bahati maarufu kama muuzaji wa mifuko ya plastiki maeneo ya stand kuu ya mabasi Bukoba amekutwa kajinyonga juu ya mti  maeneo ya ufukwe wa Spice Motel majira ya saa nane mchana .


Askari akiwa amepanda mti ili aweze kukata kamba aliyotumia kujinyongea


 Kamanda wa polisi wilaya ya Bukoba mjini akishuhudia tukio hilo
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 

 Mmoja wa watu wa kwanza kutoa taarifa kituo cha polisi Mama Faima

 Wananchi waliokusanyika katika tukio
 




 Mkuu wa kituo cha polisi Bukoba(wa kwanza kulia) akiwa anaangalia baadhi uya vitu vya marehemu alivyokuja navyo kabla ya kujinyonga


 Hivi ni vitu vya marehemu alivyokuja navyo babla ya kujinyonga












 Maeneo ya spice beach





 Mwili wa marehemu ukipakiwa kwenye gari la polisi.


Mwili wa marehemu ukipelekwa kuifadhiwa hospital ya mkoa wa kagera

Taarifa za awali  kutoka kwa watu waliokuwa katika tukio hilo zinasema  kuwa , kabla ya kifo cha, marehemu alionekana akiwa na mafurushi ya vitu na alikuwa akifua katika eneo hilo la ufukweni.

Mtu mmoja ambae hakuwa tayari kutaja jina lake  ameueleza  mtandao  huu  kuwa  leo majira ya saa 12.00 asubuhi alisalimiana na marehemu maeneo ya stand ya mabasi akiendelea na shughuli yake ya kutembeza mifuko ya plastiki kwenye mabasi yaendayo  mikoani na maeneo mengine akiwa mzima wa afya.

Mwili wa marehemu umepelekwa Hospital ya Mkoa  wa Kagera kuifadhiwa kwa ajili ya utambuzi ( ndugu zake )
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>