Ripoti nyingi za vyombo vya habari kuhusu mashindano ya Masika ya Olimpiki 2014 huko Sochi, Urusi, zinaangazia zaidi gharama zilizotumika zilizovunja rekodi katika idadi ya wanariadha wanaoshiriki, mashindano wanayoenda kushindania na vingine.
Wakati ambapo mashindano ya mwaka 2010 ya Vancouver Olympics yalifanyika kwa bajeti ya euro bilioni 5.5, waandaji wa Sochi wametumia euro bilioni 37.5 (sawa na dola bilioni 50) kwa miaka nane kwaajili ya maandalizi peke yake.
Mpaka mashindano hayo yanamazilika, euro bilioni 50 zinatarajiwa kutumika. Pesa nyingi katika hizi zilikuwa za muhimu kubadilisha eneo hilo maarufu kwa watalii hasa kutokana na mandhari yake ya bahari na pwani za kuvutia, kuwa kiwanja cha michezo ya masika.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Viwanja vya michezo hiyo vipo kwenye wilaya ya Krasnaya Polyana, kilometa 40 kutoka kwenye pwani, futi 1,969, juu ya uso wa bahari. Viwanja vyote vilijengwa kuanzia mwanzo pamoja na miundo mbinu yake.
Waandaji wamesema hadi sasa asilimia 80 ya tiketi za michuano hiyo zimeshauzwa.
Hata hivyo Marekani imetoa onyo kuwa magaidi wanaweza kuwa na mipango ya kuzilipua ndege zinazoenda kwenye mashindano hayo kwa kutumia mabomu yaliyowekwa kwenye dawa za kusugulia meno. Onyo hilo limekuja wiki kadhaa baada ya kudaiwa kuwa michezo hiyo inalengwa na magaidi.
Mashindano hayo yanazinduliwa rasmi Ijumaa hii, 7 February na yataendelea hadi tarehe 23 February 2014.