Akizungumza na Mbeya yetu Meneja Miradi wa Kituo Nuru, Osward Poyo, alisema kituo hicho ambacho hupokea watoto kutoka ustawi wa Jamii kutokana na kuwakuta watoto katika mazingira hatarishi ambapo wengi wao hawana wazazi kabisa kinakabiliwa na Changamoto ambazo wakipata msaada kwa wadau kituo kinaweza kujiendesha vizuri.
Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango, alisema kituo cha Nuru kilianzishwa Mwaka 2000 ambapo hadi sasa wameweza kupata misaada mbali mbali kutoka kwa wafadhili ikiwemo Vyakula,Majengo, Vitanda na magodoro.
Watoto hawa ni wadogo sana hukaa chini sakafuni kutokana na ukosefu wa mikeka na vifaa vya michezo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa uzio hivyo wasamaria wema mnaombwa kujitokeza kuchangia ujenzi wa uzio kituoni hapo
WADAU mbali mbali wameombwa kuchangia baadhi ya mahitaji katika kituo cha kulelea watoto Yatima cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya, kutokana na kuzidiwa na changamoto nyingi zinazokikabili.
Akizungumza na Mbeya yetu Meneja Miradi wa Kituo hicho, Osward Poyo, alisema kituo hicho ambacho hupokea watoto kutoka ustawi wa Jamii kutokana na kuwakuta watoto katika mazingira hatarishi ambapo wengi wao hawana wazazi kabisa kinakabiliwa na Changamoto ambazo wakipata msaada kwa wadau kituo kinaweza kujiendesha vizuri.
Alisema kituo hicho ambacho hadi sasa kina watoto 20 wenye umri kati ya 0 hadi 7, na wengine watatu ambao ni wakubwa wakiwa wanasoma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iringa huku wakiwa ni walemavu wa ngozi(ALBINO).
Alisema watoto hao walemavu wa ngozi walipokelewa kituoni hapo Mwaka 2000 baada ya kukimbia tatizo la mauaji ya maalbino lililokuwa limekithiri Mkoani Mbeya ambapo baada ya kulelewa vizuri na kusomeshwa hivi sasa wanasoma Sekondari na hali zao ni nzuri kabisa.
Naye Meneja wa Kituo hicho, Amanda Fihavango, alisema kituo cha Nuru kilianzishwa Mwaka 2000 ambapo hadi sasa wameweza kupata misaada mbali mbali kutoka kwa wafadhili ikiwemo Vyakula,Majengo, Vitanda na magodoro.
Alisema pia upande wa mishahara kwa watumishi katika kituo hicho hutolewa na Familia moja kutoka Uswisi lakini upande wa Serikali ambayo ndiyo hupeleka watoto katika kituo hicho hawana msaada wowote na kuongeza kuwa kazi yao ni kuokota watoto na kuwakabidhi.
Alivitaja baadhi ya vitu vinavyohitajika kwa sasa kuwa ni pamoja na Vifaa vya michezo ya kuchangamsha watoto ikiwemo Midoli, baiskeli na michezo ya Watoto,mahali pa kuchezea, Soksi kwa ajili ya kuzuia baridi na bwawa la kuogelea.
Alivitaja vingine kuwa ni Mikeka ya kukalia watoto ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na baridi kutokana na hivi sasa watoto hao ambao ni wadogo sana kukaa chini sakafuni kutokana na ukosefu wa mikeka na vifaa vya michezo.
Meneja huyo aliongeza kuwa mbali na upatikanaji wa vifaa hivyo, pia Kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa uzio ambao utaweza kulinda vitu vitakavyo nunuliwa na kuwekwa kwa ajili ya watoto ili visiibiwe na wezi pamoja na vibaka.
Mbali na hilo pia kituo hicho kinasomesha watoto 30 wanaoishi katika mazingira magumu katika chuo cha ufundi Veta Mbeya ambao wanalipiwa kutoka msaada wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Alisema watoto hao walianza masomo Novemba 1, mwaka jana wakijifunza katika Nyanja za Kilimo, Cherehani, Seremala na uchomeleaji ambapo baada ya kuhitimu masomo yao watapewa vifaa vya kufanyia kazi
Na Mbeya yetu