Baada ya kutokea kwa mtafaruko kwenye kampuni ya Microsoft baina ya Bill Gates na wawekezaji wakubwa watatu wa kampuni ya Microsoft ya Marekani kwamba aachie ngazi ya uenyekiti baada ya kukalia kiti hicho kwa miaka 40 toka ilipoanzishwa. Sasa imeleta mtazamo mwingine.
Kwa ripoti iliyotolewa na Skynews mwezi wa 10 mwaka jana zinasema kuwa wawekezaji hao wanadai kuwa uwepo wa Mr Gates katika bodi ya wakurugenzi inazuia mabadiliko ya mbinu mpya za maendeleo ya kampuni hiyo na kuweka ugumu kwa Chief executive wa sasa kufanya mabadiliko makubwa.
Bill Gates sasa amejiondoa kama mwenyekiti wa kampuni yake ya Microsoft na kushika wadhifa mpya kama mshauri wa teknolojia. Satya Nadella ametajwa kuwa mwenyekiti mtendaji mkuu wa kampuni hiyo.
Tangazo la CEO mpya limekuja baada ya aliyekuwepo Steve Ballmer kutangaza mwaka jana nia yake ya kustafu.
Nadella anakuwa mwenyekiti mtendaji wa tatu katika historia ya miaka 39 ya Microsoft, baada ya mwanzilishi mwenza Bill Gates na Steve Ballmer.
Microsoft imesema John Thompson atachukua nafasi ya uenyekiti iliyoachwa na Bill Gates.