Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WAUZA NGUO ZA NDANI MITUMBA WAIZIDI UJANJA TBS

$
0
0

WAFANYABIASHARA wa nguo za ndani zilizo hafifu maarufu kama mitumba jijini Mbeya, jana waliwazidi ujanja maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kuficha nguo hizo wakati wa operesheni ya kuzikusanya na kuwakamata wauzaji.
Wafanyabiashara hao walioonekana kupewa taarifa ya nini kitafanyika kabla walificha nguo hizo hatari kwa afya za wavaaji na baada ya kumalizika kwa uparesheni wakazirejesha sokoni na kuendelea kuziuza kama kawaida huku wakijigamba kuwa Serikali haiwawezi.
Awali maofisa wa TBS walioambatana na askari wa Jeshi la Polisi na waandishi wa habari, waliendesha operesheni ya kukamata nguo za ndani hususani chupi, sidiria na soksi katika masoko ya Sido na Mwanjelwa lakini hawakufanikiwa kukamata hata nguo moja katika masoko hayo yaliyo maarufu kwa uuzaji wa nguo za mitumba ikiwemo zilizokuwa zikitafutwa.
Ajabu ni kuwa wafanyabiashara hao walionesha kuwa na taarifa ya kufanyika kwa operesheni na kila kona ya masoko hayo walisikika wakizungumza kuwa maofisa wa TBS na polisi wako katika eneo lao wakifanya operesheni ya kukamata nguo hizo.
“Umewaona ndio hao wamekuja kwa ajili ya kukamata zile nguo. Lakini wanatafuta tu ukorofi kama wanataka kukamata nguo za mitumba si wakamate tu na mashati basi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
“Kwa nini watilie mkazo kwenye nguo za ndani pekee?” Walisikika wafanyabiashara katika baadhi ya vibanda vya masoko hayo mawili wakihoji hali iliyoonesha kuwa hawana elimu ya kutosha juu ya athari za kuvaliwa kwa nguo hizo.
Mahali pekee walikofanikiwa maofisa hao ni katika Soko la Mbalizi ambako walifanikiwa kumkamata mfanyabiashara mmoja Lusekelo Adam akiwa anauza soksi za mtumba na kumfikisha ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya na kisha kuteketeza soksi hizo ambazo muuzaji alisema zilikuwa na thamani ya Sh 200,000.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa operesheni hiyo Ofisa Viwango na Mkaguzi wa TBS, Paul Manyirifa alikiri zoezi hilo kufanyika kwa wafanyabiashara walio wadogo na kusema shirika linaamini wapo wafanyabiashara wakubwa ambao ndio huziingiza kwa njia za panya na kuwataka wajisalimishe.
Kwa upande wake Mwanasheria wa shirika hilo, Baptista Bitao alisema adhabu kwa mtu yeyote anayeuza nguo hizo ni kati ya Sh milioni 50 hadi 100 lakini pia Mkurugenzi Mkuu wa shirika ana mamlaka ya kutoa adhabu isiyopungua Sh milioni 20.
Naye Kamanda wa Polisi mkoani hapa Ahmed Msangi aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kina kukamata nguo hizo akisema lengo ni kuona Watanzania hawawi watu wa kupokea vitu vitakavyolisababishia hasara Taifa lao kwa kuingia gharama ya kutibu maradhi yatokanayo na nguo hizo.

HABARI LEO

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>