BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilichoanza rasmi tarehe 1 Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEEna Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT kitaishia tarehe 28 Februari, 2014.
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.