Akizungumza kwa njia ya simu Ripota wa Mtandao huu, alisema kuwa, Viongozi hao wa Chadema, wamekamatwa na Polisi leo asubuhi na kuwashikilia kwa muda kituoni hapo wakihojiwa baada ya jana kupitisha muda katika mkutano wao waliofanya mkoani hapo.
Aidha imeelezwa kuwa viongozi hao walichelewa kufika eneo la mkutano baada ya Rubani wao kupotea angani na kufika eneo hilo zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya muda wa mkutano kumalizika, jambo lililomfanya mwenyekiti huyo kuwaomba Polisi wasimamizi wa usalama kuongea japo kwa dakika chahe ili kuwajulisha wanachama wao kilichotokea.
Baada ya kuruhusiwa kufanya hivyo imedaiwa kuwa mwenyekiti huyo aliyekuwa ameongozana na wabunge wake wawili, alipitisha muda na kuzua maswali miongoni mwa wanausalama wa mkoa huo, jambo lililowapelekea kukamatwa na kuhojiwa kwa muda kituo cha Kati mkoani Iringa leo majira ya saa tatu asubuhi na baadaye kuachiwa wakaendelea na safari zao.