Sehemu ya Kwanza (madhara, kiafya, kikazi na majukumu)
1. Kiafya
Kuripoti kwa bosi mtata au mbaya inakughalimu nguvu nyingi kuliko vile unavyofikiri kama unafanya kazi kwa masaa nane kwa siku au siku tano kwa wiki. Ukijikuta kwenye hali ngumu kikazi ,utakuwa na kazi mara mbili ili uweze kufanya kazi vizuri na vile vile kupambana na ukatili au unyanyasaji eneo hilo la kazi kitu ambacho utakifanya kwa muda wako.
Uwe makini mawazo yako au fikira zako zisikudanganye. Hakuna mtu ambaye anaweza kustahimili manyanyaso ya kifikra, na kisaikolojia kwa muda mrefu bila kukumbana na madhara kama, msongo wa mawazo, kushuka moyo, kushindwa kufanya kazi, kupoteza mwelekeo wa kile unachopaswa kufanya kazini, vilevile kupoteza uwezo na umakini wa kufanya jambo moja kwa muda mrefu.
Haijalishi unajifanya unaweza kustahimili kwa muda mrefu, jitahidi manyanyaso ya bosi huyo mbaya au mtata yasiende zaidi ya wiki nne. Utakapokuwa na msongo wa mawazo, utapoteza nguvu nyingi ili upambane na hali hiyo. Jaribu kujitizama mwenyewe kama kuna dalili fulani kama hizo.
Kuwa makini kuwasikiliza ndugu na jamaa ambao mara nyingi wanakuuliza ‘wewe tatizo ni nini?’ unafikiri unaweza kutenga mambo ya kazi na maisha yako binafsi, bali ukishambuliwa kisaikolojia kama mabosi watata wanavyofanya mambo hayo yatakufuata kazini na nyumbani kutatokea madhara yake.
Kama unafikiri ndani yako huhitaji msaada, labda hahuhitaji msaada lakini unahitaji msaada. Tafuta mwanasaikolojia ambaye atakusaidia kuongeza nguvu na uwezo wako kihisia ili kuboresha hali yako.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
2 Kazi nyingi Haimaanishi majukumu zaidi
Mabosi watata au makatili au wabaya hunufaika na mazingira fulani kwa wafanyakazi, anakupa kazi nyingi zaidi ya zile unazohitajika kufanya badala ya kukuongezea majukumu ambayo yataweka changamoto katika utendaji wako. Na vile vile wanakuongezea majukumu bila kuongeza mshahara wako.
Kama wewe una majukumu ya kila siku na ukapewa kazi kubwa inayohitaji ujuzi zaidi na ni zaidi ya majukumu yako ya kazi kulingana na mkataba, unaweza kuwa unafanya kazi katika nyadhifa ya juu sana kuliko mshahara wako. Ingawa ukipewa jukumu kubwa ni fursa wa wewe kujifunza ujuzi mpya na inakuandaa katika hatua nyingine kubwa zaidi, hiyo inafaida kama; semina na mafunzo ya hapa na pale ambayo hayaendani na kuongezewa mshahara.
Kama bosi huyo ana mpango wa kukuendeleza kiutendaji, atakusaidia na kukuelekeza namna ya kufanikisha ila hata kuacha uhangaike nalo. Akikuacha ufanye mwenyewe halafu anataka matokeo mazuri huyo anampango wa kukuangusha. Kukuongezea majukumu kunaongeza uthamani wa kazi yako, na kwa muda fulani inaongeza faida ya kiwango cha mshahara kuongezeka na mambo mengine.
3. Pata nakala ya majukumu yako kikazi
Mshahara wako unatokana na majukumu yako na wajibu uliopewa kazini. Hivyo majukumu yako kikazi yanategemea ujuzi ulionao ambayo yameelezewa kwenye nakala ya majukumu unayotakiwa kufanya. Unapoyatekeleza yanatakiwa kulipwa kwa mshahara uliopangwa.
Nakala yako ya majukumu kikazi ni muhimu kuwa nayo. Majukumu hayo yanaelezwa bayana kwenye mkataba “kutoka siku hii, majukumu yako ni……… na utalipwa kiasi kadhaa” Hivyo usipokuwa na nakala ya majukumu yako, utakapoambiwa ufanye kazi fulani itakuwa ngumu kujua unatekeleza kulingana na vile utakavyolipwa au ni zaidi ya majukumu yako na kusababisha kutumiwa vibaya na mwajiri wako bila ya wewe kujua.
Ni haki yako kuomba nakala ya majukumu yako pale unapoanza kazi kabla changamoto hazijaanza kuibuka. Bosi wako asipokupatia kazitafute kwa afisa mwajiri, hasa kwa taasisi kubwa. Zile taasisi ndogo wanaweza wasiwe nazo ila waambie wakutengenezee na kukuandikia kuna wakati wanasema majukumu mengine kama utakavyopangiwa na bosi au msimamizi, tafuta kujua na wakwambie hayo majukumu mengine ili kujua yanaendana na kiwango cha mshahara wako?
Kumbuka kama haijaandikwa ‘ni kwamba haipo’.