Watengenezaji wa komputa wa nchini China, Lenovo wamezinunua simu za Motorola kutoka kwa Google. Google imethibitisha kupitia website yake kuwa imeiuza Motorola kwa gharama ya dola bilioni 2.91.
Lenovo itapewa brand ya Motorola pamoja na simu zake zikiwemo Moto X na Moto G. Kwa kuongeza, itapewa zaidi ya haki miliki za teknolojia 2,000 huku Google ikiendelea kusimamia haki miliki nyingi ilizozipata baada ya kuinunua Motorola miaka kadhaa iliyopita.
Dili hiyo inaipa Lenovo, yenye biashara ya smartphone iliyofanikiwa nchini China, brand inayofahamika kimataifa.
Hata hivyo Google ndio iliyopata hasara kwenye biashara hiyo kwakuwa mwaka 2011, iliinununua kampuni ya Motorola Mobility kwa dola bilioni 12.5.