Dereva nyota wa zamani wa mashindano ya magari kutoka Ujerumani, Michael Schumacher bado hali yake ni mbaya na madaktari wanaendelea kumweka katika hali ya ‘kuzirai kimatibabu’
Meneja wake ameiambia BBC kuwa madaktari wanaendelea kumweka katika hali ya ‘kuzirai kimatibabu’ wakijaribu kupunguza uvimbe na kuchubuka kwenye ubongo wake ambapo wametekeleza upasuaji mara mbili kuondoa damu iliyoganda kwenye ubongo.
Hata hivyo huenda maisha yake yakawa hatarini iwapo ataendelea kuwa katika hali ya kuzirai kutokana na hatari ya ubongo wake kuharibika na kupata maambukizi ya kifua.
Bingwa huyo mara saba aligonga kichwa chake dhidi ya mwamba wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Source:BBC