Huu ndio mwonekano wa Gari aliyokuwa akiendesha Mh. Ngasongwa.Picha na Chriss Mfinanga.
Mh. Ngasongwa akisaidiwa na muuguzi wa Hospitali ya Tumbi.
Hii ndio gari iliyosababisha ajali hiyo.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharib, Mh. Juma Ngasongwa amenusurika kifo katika ajali iliyotokea jana jioni maeneo ya Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani.
Ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Rav 4 mali ya Mh. Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam wakati akielekea Mkoani Morogoro, ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Shirika la Umeme (Tanesco) lenye Namba za Usajili SU 37199 na kupelekea kutokea kwa ajali hiyo.
Mh. Ngasongwa alikimbizwa Hospitali ya Tumbi,Kibaha na kuanza kupatiwa matibabu mara moja na baadae alihashiwa Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili katika taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.