Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

ZIFAHAMU DALILI ZA KWAMBA UNAKABILIWA NA UBAGUZI KAZINI

$
0
0
Hakuna mtu anayependa mazingira magumu ya kazi. Ingawa kama unaamini hali ya ubaguzi ipo au lah, mara nyingi ni vigumu kuigundua moja kwa moja. Hivyo kuna baadhi ya tabia za kikorofi au unyanyasaji ambazo ni vigumu kujua kama unanyanyaswa kikazi au ni jambo binafsi.

Je unakumbana na ubaguzi kazini? Hizi ni dalili za kujua kama unabaguliwa

Watu wengi wanaacha kazi
Kama kampuni au shirika linaendelea kwa nguvu kuajiri watu wengi inamaanisha watu wengi wanaacha kazi, hii inaashiria wafanyakazi hawapendezwi na mazingira ya kazi. Ingawa watu kuacha na kuanza kazi si kigezo pekee cha ubaguzi makazini, kwakuwa watu wengi wana kiwango cha juu cha uvumilivu hata kama mazingira ni mabaya. Kama wafanyakazi wanaacha kwa mkupuo muda si mrefu baada ya kuajiriwa hapo inamaanisha kuna tatizo kubwa. Wafanyakazi wanapaswa kufungua macho na kujua.

Maswali ya utata wakati wa Usaili
Ubaguzi wa kikazi huanza wakati wa Usaili unapoendelea. Ukiona msaili wako unauliza maswali ambayo yanaendana na mlengo fulani, labda dini, rangi, kabila au taifa kuna uwezekano mkubwa wa kutohusiana vizuri na wewe hata akikuajiri. Mashirika na makampuni mengi kisela yanaruhusu watu wa aina tofauti tofauti na imani tofauti ingawa sio mameneja wote wanaokubalilana na hali hiyo. Hivyo inamaanisha kwamba watu wa mlengo mmoja na bosi au mwajiri huajiriwa kirahisi sana. Igawa udhalilishaji(kijinsia na kihisia) na maonezi hutokea wakati umeanza kazi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Utaratibu mbaya wa kupanga kazi kwa wafanyakazi
Wafanyakazi wanaotengwa hupewa kazi ndogo au chache zisizo na tija ama wakati mwingine hupewa kazi ngumu zisizoisha kirahisi. Mkakati huu unakuwa kuwatengenezea nafasi wale ambao ni wa mlengo wake ambao mara nyingi hawana uwezo wa kufanya kazi ila hupandishwa vyeo na kuongezewa mishahara na wakati mwingine kutengeneza mazingira ya kumachisha kazi mfanyakazi anayetengwa.

Namna ya mazungumzo yanavyofanyika na mabosi
Sehemu nyingine ya kutengwa kazini huhusisha namna kiongozi au bosi anavyoongea na mtu asiyempenda au kutomtaka. Kama mara nyingi unafokewa na kusemeshwa kwa ukali bila sababu tambua ya kuwa kuna kitu kinaendelea. Wakati mwingine utani usiokuwa wa manufaa kwako. Na mambo haya hulenga hasa dini, kabila, & umri.
Kama unahisi mambo si ya kawaida kazini kwako, jaribu kuomba ushauri na vilevile mwanasheria au taasisi inayohusika na matatizo kazini kwa msaada zaidi. Usijaribu kushughulikia tatizo peke yako.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles