Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UPDATES: MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU IMEWAACHIA HURU MENEJA UENDELEZAJI BIASHARA WA MWANANCHI COMMUNICATIONS (MCL)

$
0
0
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda akiongea na waandishi baada ya kushinda kesi katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd,Tido Mhandoa kiongea na waandishi wa habari baada ya hukumu.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru  Meneja Uendelezaji Biashara wa Mwananchi Communications (MCL), Theophil Makunga, aliyekuwa Mhariri Mtendaji  wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Waliarwande Lema amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa makala iliyoandikwa na Mwigamba na kuchapishwa Tanzania Daima ilikuwa ya uchochezi, habari kamili na undani zaidi kesho.
Hukumu ya kesi ya kina Makunga leo
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi inayomkabili Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga na wenzake wawili.

Katika kesi hiyo, Makunga ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda na Mwenyekiti wa zamani wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Kwa pamoja, washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa majeshi ya ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye Gazeti la Tanzania Daima ikiwa na maneno yanayodaiwa kulenga kuwashawishi wasiwatii viongozi wao.
Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema anatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka na utetezi kumaliza kutoa ushahidi wao na kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho. Hata hivyo, upande wa mashtaka haukuwasilisha majumuisho.
Awali, kesi hiyo ilianza kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuwaita mashahidi watatu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo - Usajili wa Magazeti), Raphael Hokororo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza (ACP), George Mwambashi kutoka Kitengo cha Sheria cha kikosi hicho na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), David Hizza.
Baada ya washtakiwa kumaliza kutoa ushahidi wao, Wakili wa Serikali, Beatha Kitau alifunga ushahidi, Mahakama ikaupitia na kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu.
Makunga na wenzake, Absalom Kibanda na Samson Mwigamba walifunguliwa kesi hiyo baada ya kuchapishwa kwa makala hayo Novemba 30, 2012 yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi yakiwa na kichwa cha habari ‘Waraka maalumu kwa askari wote.’
Makala hayo yaliandikwa na Samson Mwigamba kupitia safu yake ya ‘Kalamu ya Mwigamba’ katika gazeti hilo. Makunga anashtakiwa kama mchapishaji kwani makala hayo yalichapwa na Kiwanda cha Uchapishaji cha Mwananchi Communications Ltd, wakati huo akiwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Kibanda ameshtakiwa kutokana na wadhifa wake wa mhariri wa gazeti lililochapisha makala hayo.
Washtakiwa hao wanatetewa na mawakili Nyaronyo Kicheere, John Mhozya, Frank Mwalongo na Mabere Marando.
MWANANCHI

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles