Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UNATAKA KUENDESHA BIASHARA YAKO? HAYA NI MAMBO YA MSINGI KUZINGATIA

$
0
0
 Je una kila kitu cha kukuwezesha kuendesha biashara yako? Fuatilia vitu hivi kujua uwezo wako.
Je Una mawazo ya kibiashara ya kueleweka?
Wazo la kibiashara linahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri na utafiti. Wazo hilo lazima liendane na kutimiza haja ya soko lililopo na kuliboresha. Mawazo bora yanatokana na utafiti makini, weledi madhubuti katika nyanja ya ujasiriamali.

Je unajua washindani wako kibiashara?
Unaweza kuwa unajua kinadharia. Hii inamaanisha watu waliokwenye mlengo mmoja na wewe kibiashara. Mara nyingi hakuna ushindani wa moja kwa moja, bali inamaanisha watu badala ya kununua bidhaa yako au huduma yako wanakwenda kununua sehemu nyingine.

Je Unapataje fedha ya kuendesha Biashara yako?
Fedha au Mtaji wa biashara ni kitu kikubwa ambacho kinahitajika kuanzisha biashara nyingi afrika na hapa nchini. Uzuri wa jambo hili ni kwamba taasisi nyingi za fedha zimekuja na huduma za fedha ambazo kwa kiasi fulani kuweza kutoa mitaji midogo, mikopo na hata mitaji ya Amali n.k

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Je una ujuzi wa Biashara?
Unapoingia kwenye biashara ambayo huna ujuzi nayo ni kosa kubwa na unajiingiza kwenye matatizo ambayo yataathiri hiyo biashara na mtaji wako. Jifunze kuhusu hiyo biashara kabla ya kuanza kuifanya.

Je umejiandaa kufanya kazi kwa juhudi?
Watu wengi hushitukizwa kwamba masaa ya kazi huongezeka kama ndo unaanza kuianzisha biashara yako. Ukijua hila utaweza kupambana na changamoto za hapa na pale.

Nani atasimamia mambo ya fedha?
Mahesabu huwa yanaongea. Hivyo ajiri au weka mtu atakaye kusaidia kufanya hiyo kazi au kampuni ya kuangalia mahesabu ya fedha. Kuhakikisha nyaraka zote ziko za malipo ,kodi na uagizaji ziko sahihi. Weka fedha ya ziada itakayokusadia kibiashara endapo biashara itayumba.

Je mpango wako umekaaje?
Ifanyie kazi biashara badala ya kufanya kazi za kila siku kama kuuza. Simamia mambo ya kupanga bei, angalia gharama ulizotumia kuleta huo mzigo, soko limekaaje halafu madhara ya bei hiyo katika biashara yako. Simamia mpango mkakati wa biashara yako wa muda mrefu labda miaka mitatu ijayo, mitano hadi kumi na kuendelea. Je mpango wako wa utafutaji masoko umekaaje? je utawashawishi vipi watu kuhusu biashara yako? Ongelea biashara yako mahali popote unapokuwa.

Mwonekano wako unasemaje kuhusu wewe?
Hivyo hivyo kwenye biashara, Je jina la biashara likoje? Biashara yako iko wapi? Je inafikika na wateja, usalama upo, je washindani wako wapo wapi? Je nembo yako ikoje?

Je umejipanga kuboresha?
Kuna mambo mengi yanaendelea ulimwenguni, mabadiliko ya kila namna na soko la jana haliwezi kuwa la kesho. Unahitaji ubunifu na mpango wa kuboresha kila siku.

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>