Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

KITALE ASEMA MUZIKI UNALIPA ZAIDI NDIYO MAANA WASANII WA MAIGIZO WANAKIMBIA KUUFANYA

$
0
0
Msanii wa maigizo na muziki Kitale amesema watu wasije kushangaa kuona wasanii wengi wa maigizo wanaingia kwenye muziki kwasababu unalipa mara 10 zaidi ya filamu.
Akizungumza na mtandao huu leo Kitale amesema kazi za filamu zinamzunguko mkubwa mpaka kupata mafanikio ya pesa, ndiyo maana wasanii wengi wa maigizo baada ya kupata majina huingia katika muziki ili kujipatia kipato kwa haraka.
“Muziki una hela kuliko maigizo lakini ukiwa mbali na muziki huwezi kujua, wapo watu wanaamini maigizo yanalipa kuliko muziki,lakini Kitale yupo kwenye maigizo na muziki,maigizo yanachukua muda ila unaweza ukauza kwa milioni 15,20 mpaka 25 ndani ya miezi mine au mitatu, hapo bado haujazungukia bodi ya filamu sijui wapi,kwahiyo mambo yanakuwa mengi sana. Lakini muziki unaweza ukapata wazo wakati umelala, ukakesha studio ukafanya ngoma kali,ukasambaza ukabaki unasubiria show ,kwahiyo unawaona wasanii wa maigizo wanaimba ni kwa sababu muziki unalipa mara kumi ya filamu”.
Aliedelea kusema,

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

“Kitale kama Kitale maisha yangu yote kwa sasa nategemea muziki kuliko maigizo, nikipata show zangu mbili kwa milioni 6,kila show milioni tatu nakuwa mjanja, hiyo labda ni ndani ya mwezi mmoja wakati ilamu ni miezi mitatu, kwahiyo sikufichi kwenye filamu hakuna kitu ndiyo maana wasanii wa kuigiza wengi wameingia kwenye muziki” Alisema Kitale.

SOURCE: BONGO 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>