Michuano ya kombe la FA imeingia raundi ya tano ambapo mechi zote zitachezwa Jumamosi na Jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi pili huku Chelsea na Manchester City zikitazamiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Chelsea walifuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila. Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii alisema: Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora.”
Pia Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2
Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano,huku Roberto Martinez akiiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi iliyokutanisha timu zote za ligi ya England.
Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton. Sheffield watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.
Mshindi wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainali yake itachezwa kwenye uwanja wa Wembley.
Source:BBC
Source:BBC