Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
Askari wa hifadhi ya mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamesimama wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Askari wa hifadhi ya mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu.
Picha na Katavi yetu Blog
*********************
Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog.
Mpanda Katavi
Jumla ya Askari 96 wa Shirika la Hifadhi la Taifa la Wanyama Pori (TANAPA) wametimu mafunzo ya miezi mitatu katika chuo kipya cha wanyama pori cha Mlele kilichopo Mkoa wa Katavi na kutoa kiapo cha uti mbele ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi
Askari hao wa TANAPA walimaliza mafunzo hayo hapo juzi kwenye chuo hicho cha wanyama Pori cha Mlele akiwa ni mafunzo ya kwanza hapa nchini kwa TANAPA kutoa mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo kabla ya kuanza kazi
Katika Risala yao ya wahitimu wa mafunzo hayo ya kulinda maliasili iliyosomwa na Bruno Mbunda walieleza kuwa wamejifundisha mbinu mbalimbali za kulinda rasilimali za Taifa kwa Vitendo na nadharia
Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata waharifu kumpekua mharifu na kutotumia nguvu sana katika kukamata mharifu pamoja na pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha
Walieleza katika kipindi hicho cha mafunzo wahitimi hao walifanikiwa kukamata waharifu hamsini wakati wakifanya doria katika maeneo mbambali ya Mbuga ya Katavi na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi
Wahitimu hao walieleza kuwa mafunzo hayo yaliwashirikisha Askari 99 lakini watatu kati yao wameshindwa kuhitimu zikiwemo sababu mbambali kama utoro na utovu wa nidhamu hari ambayo ilfanya wahitimu waliomaliza kubaki 96 ambapo kati yao mwanamke ni mmoja na wanaume ni 95
Kwa upande wake mkuu wamapori ya akiba ya Rukwa Lwafi Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano na ubovu wa miundo mbinu ya barabaa na upungufu wa magari pamoja idadi ndogo ya washiriki wa mafunzo kwa wanawake na ufinyu wa bajeti
Nae Mkurugenzi wa Hifadhi na Ikolojia Martini Loibook alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata yanaumuhimu sana hasa kutokana na changamoto zinazoikabili nchi yetu inayokabiliwa na wimbi la ujangili
Pia Mkurugenzi wa utumishi na utawalla wa TANAPA Witnes Shoo aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa uaminifu kwa kujituma na wawe na didamu na wasiwe na tabia ya kutow a siri za ofisi
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliwaasa wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu mkubwa hasa katika shughuli zao katika kupambana kukomesha ujangili
Aliwataka kutojihusisha na masuala ya ujangiri na badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo ndani ya nchi na nje ya nchi
Alisema wapo baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kueubuniwa na mtu yoyote yule au watu