Baadhi ya wananchi wa mji wa Mbeya wakiwa wabeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima wa Chadema, uliofanyika kwenye Uwanja wa Lwanda Nzovwe mjini Mbeya jana.
Mbunge wa Mbozi Mashariki, Davi Silinde (Chadema), akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe mjini Mbeya jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, wakiondoka kwa shamrashamra, baada ya kuhutubia mkutano wa hadahara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwa amembeba mtoto Sheila Shukurani (3), kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara matika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya na vitongiji vyake katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana.
Picha na CHADEMA