Sandro Rosell
Rais wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell, amejiuzulu kufuatia madai ya utumizi mabaya ya fedha wakati klabu hiyo ilipomsajili nyota wa Brazil, Neymar mwaka uliopita.
Rosell, amesema madai yanadhamiria kumharibia sifa na kuwa sio ya kweli lakini amehisi hadhi ya heshima ya klabu hiyo itahujumiwa ikiwa ataendelea kuhudumu kama rais wa klabu hiyo.
“The Board of Directors is a team. And this team leads a project that has brought the Club great success. I don’t want unfair attacks to negatively affect their management or the image of the Club. This is why I think my time here has come to an end. Now, in accordance with the Club’s Statutes, I have presented my irrevocable resignation of the presidency of FC Barcelona to the Board of Directors,” alisema Sandro.
Mapema wiki hii, gazeti moja nchini Uhispania liliandika kuwa klabu hiyo ilitumia Euro milioni 40 zaidi kuliko ilivyotangazwa kumsajili mchezaji huyo kutoka Brazil. Ripoti zinasema kuwa baba yake na Neymar na mawakala wengine waliohusika na mkataba huo walilipwa kiasi fulani cha pesa ambacho hakikutangazwa.