Mpenzi wa siku nyingi wa mmiliki wa club ya Chelsea na bilionea wa Urusi, Roman Abramovich aitwaye Dasha Zhukova,ameomba radhi kwa picha yake inayomuonesha akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa umbo la mwanamke mweusi aliye nusu mtupu.
Picha hiyo iliyokuwa imewekwa kwenye interview aliyofanyiwa na mtandao wa masuala ya mitindo wa Buro247.ru, ilisambaa Jumatatu hii wakati ambapo Wamarekani walikuwa wakisherehekea siku ya Martin Luther King Jr. Day aliyekuwa mtetezi wa watu wamarekani wenye asili ya Afrika.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Picha hiyo ilipunguzwa na kumuonesha Zhukova na sehemu tu ya kiti hicho baada ya kuleta mjadala mkubwa mtandaoni kutokana na kuwa kibaguzi.Kwenye maelezo yake yaliyochapishwa na gazeti la The Moscow Times, Zhukova alisema kutumika kwa picha hiyo ni kitendo cha kujuta hasa katika siku ya Martin Luther King Jr na kwamba yeye si mbaguzi wa rangi.
Sehemu ya maelezo yake inasomeka: This photograph, which has been published completely out of context, is of an art work intended specifically as a commentary on gender and racial politics. I utterly abhor racism, and would like to apologize to anyone who has been offended by this image
Wanaharakati mbalimbali wamemtuhumu Zhukova kuwa anapigia debe utumwa.