Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

JE UNATAKA KUBADILISHA TAALUMA YAKO? EPUKA MAKOSA HAYA

$
0
0
 
Kama kocha wa mambo ya taaluma, ninaweza kukwambia suala la kubadilisha taaluma ni kitu kinachohusiana sana na maadili yako, mahitaji yako, ujuzi na vitu unavyovipenda hata katika kipindi hiki ambacho hali ya uchumi si nzuri. Ukitaka kubadilisha taaluma yako ili iwe na matokeo mazuri na yenye mtizamo chanya unahitaji mambo manne ya msingi; Unahitaji maelezo yanayojitosheleza, Ujasiri, Uthubutu na uwezo. Bila vitu hivyo utahangaika na utashindwa.
Kwahiyo unapotaka kuchukua maamuzi ya kubadili kazi ama taaluma yako hakikisha kwamba hisia zako ziko imara, hali yako ya kiuchumi imetulia na kielimu. Utapitia ngazi tofauti hivyo unahitaji umakini na uelewa wa kitu unachokifanya, unahitaji kuondoa mambo ya kuiga na kufuata mkumbo. Unapaswa kujiuliza je mpaka hapa nilipofika kitu gani cha msingi ambacho nimeweka kukifanya katika taaluma yangu? Changamoto gani nimepitia na je ninawajibika vipi katika nafasi niliyonayo sasa?. Hivyo unapofanya uamuzi vitu hivi vitano uvifuate kwa makini kwa kuwa vitaathiri maisha yako, Mahusiano yako, afya, fedha na maisha yako ya baadaye.
Makosa hayo ni kama yafuatayo

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

  1. Athari za kukimbia, kukimbia taaluma uliyonayo kwa sababu umevunjika moyo na kama umesubiri muda mrefu kufanya mabadiliko ya hali yako ya sasa, umetengeneza mazingira ya kuichukia kazi yako, watu unaofanya kazi nao, kazi unayofanya na ujuzi unaotumia na unataka kukimbia mbali kabisa na taaluma hiyo. Kuna watu huwa hawaelewi kwanini wanafanya hicho wanachokifanya, na wanafanya kwa kusudi gani na mara nyingi hujaribu kukimbiakimbia kwenye taaluma. Hivyo kuishi kulingana na cheo au weledi alionao na kujikuta katika giza wa uitumia semina na mafunzo mbalimbali ili kuweza kuishi kila siku na kama dawa ya kuimarisha weledi huo. Hiyo imesababisha watu kuishia wasikokutaka. Hivyo huhitaji matengenezo mapya kitaaluma kwasababu wamekuwa wakishi kulingana na watu wanavyokwenda. Usisubiri mpaka umechoshwa na hali uliyonayo sasa ili kufanya mabadiliko. Fanya maamuzi ya kujua taaluma yako sasa. Kufanya mambo yako yaanze kwenda vizuri anza kurekebisha mahusiano yako yaliyovunjika, tengeneza heshima, tafuta sauti yako,kuza ujuzi ulionao na ongeza uwezo wako kiujuzi. Hivyo ukiondoka hapo unakuwa na uwezo wa kwenda ngazi nyingine na itakuwa wazi kwako na kusonga mbele bila matatizo. Kukimbia hapo ulipo hautarekbisha matatizo yako ila yatajirudia kwenye taaluma nyingine ambayo unaiendea.

    Kutokuwa na mpango madhubuti kiuchumi ambao utakutegemeza wakati wa mabadiliko.
    Kuna watu wengi wanahitaji mabadiliko ya taaluma lakini hakuna fedha za kufanya hivyo wala mahali watakapo pata msaada. Hivyo hawafanyi uchunguzi itamgharimu kiasi gani kufanya mabadiliko hayo na hawana fedha za kufanya mabadiliko hayo. Huweza kupata mshahara mara mbili au tatu zaidi unapokwenda kwenye taaluma nyingine inahitaji muda wa kutosha na juhudi ya ziada. Tafuta ushauri na hakikisha unaweza pata fedha za kukuwezesha kufanya mabadiliko na punguza matumizi ya fedha kwenye mambo yasiyo ya msingi.

    Kukimbilia kazi ambayo huna uhakika kama una uwezo nayo au ndio unayotaka
    Swali unalohitaji kujiuliza nina ujuzi gani na kipaji gani nataka kukitumia? Je ni jambo gani ninahitaji kusaidia? Je ni watu gani na mazingira gani na tamaduni gani ninaweza kufanya kazi nao ? Nina utu wa namna gani, nina maadili gani ambayo yatanisaidia katika kazi au taaluma hii? Nitakutana na changamoto gani katika taaluma hii? Kuna faida gani ambazo hazihitaji mjadala katika taaluma hii? Je ninataka kufika wapi na taaluma hii? Je inaendana na maisha na taratibu zangu za kuishi?

    Kutofanya utafiti wa kutosha, mfano umekuwa karani kwa miaka mingi sasa unaona muda wa kustaafu umefika unaamua kuingia kwenye ufugaji. Je umefanya utafiti wa kutosha kufanya ufugaji?Je una ujuzi kuhusu ufugaji? Na je taaluma yako inaendana na kitu unachotaka kufanya? Utahitaji kujifunza upya kuhusu ufugaji na namna mambo yanavyokwenda. Kwasababu umetumia muda mwingi kuishi maisha tofauti na unayotaka uanze kufanya sasa.

    Kukata tamaa mapema, kushindwa kufanya mabadiliko kitaaluma kunahusisha kukata tamaa mapema, huwezi kufanya mabadiliko bila kuweka jitihada ya kutosha, muda, kujitoa na kutumia fedha. Watu wengi hutegemea mabadiliko kutokea haraka sana labda kupanda cheo kwa sababu amekuwa kazini muda mrefu na vitu kama hivyo. Hivyo hukata tamaa na kutafuta mtu wa kumlaumu bila kujitizama kwamba wao wamefanya juhudi gani katika taaluma?

    Je wanajua wapi wanakwenda au wanakwenda kwa sababu watu wanakwenda? Tumekuwa na watu wengi ambao wanataka kubadili kazi au taaluma bila kufanya uchungui wa kutosha. Jaribu kuangalia maisha yako na mabadiliko ya kitaaluma unayotaka kufanya kwa kufanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kufanya mabadiliko hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>