Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

KWANINI WAFANYAKAZI HAWAWAAMINI VIONGOZI WAO? HIZI NDIZO SABABU SABA(7) ZINAZOPELEA TATIZO HILI

$
0
0
Wakati dunia ilikuwa ikiomboleza kuondoka kwa Nelson Mandela na kumkumbuka yeye kama kiongozi mahili duniani, kitu ambacho kinaonekana wazi kwa Mandela ni imani ambayo watu walikua nayo juu yake.
Viongozi wengi wakubwa duniani ilibidi wamkubali kwa kuwa mzee Mandela alinuia kuleta amani, ustawi wa jamii za watu na umoja si Africa ya kusini tu bali ulimwenguni kote. Mandela aliweza kuongoza watu kwa kiasi kwamba watu wengine inakuwa vigumu kufanya kama alivyoweza kufanya. Kama msemo wake maarufu ya kwamba “sikuzote jambo huonekana haliwezekani mpaka limewezekana”
Cha kustaajabisha ni kwamba Imani juu ya viongozi siku hizi ni vigumu kupata, watu wanamatatizo mengi kiasi kwamba hawaaminiani hata kidogo.
Kitu hicho hicho ndicho tumekileta makazini, wafanyakazi wanataka viongozi wao au watu wanaowaongoza wawe waaminifu na wawazi. Wafanyakazi wengi wamechoshwa na matokeo yasiyotarajiwa makazini kutokana tu na kutojipanga na kujiandaa vyema. Wafanyakazi wanahitaji kujua endapo mabadiliko ya kinyazifa makazini yanapotokea kabla na si baada ya vitu kugundulika kuwa haviendi sawa. Wafanyakazi wengi wanategemea kujua kitu gani kinatarajiwa kwao na kupewa nafasi ya kuonyesha ujuzi na ufanisi wao kuliko kila wakati kuambiwa kitu gani cha kufanya na kuwaona hawana vigezo vya kufanya kazi au kuchukua nyazifa Fulani hivyo huvunjika moyo.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Viongozi wengi wanatiwa changamoto kati ya kutoa taarifa za ukweli wote na kuficha baadhi ya mambo ili wasiwatishe watu au kupoteza ujuzi wa hali ya juu wa watu fulani. Viongozi wengi wako katika hali tete au hawajui nini cha kufanya kwa sababu wanajaribu kulinda kazi zao wakati huohuo wanajaribu kuonyesha imani na stahiki kwa wafanyakazi wao.Kutokana na hali hiyo ya kutoaminiana kazi ya viongozi na wafanyakazi makazini kunaleta changamoto za kiutendaji na kufanya matokeo yasiyotarajiwa kuwa kama kitu cha kawaida makazini.
Hivyo basi viongozi wamepoteza uhalisia wao na utendaji kukwama kwakuwa wafanyakazi walio chini yao hawawaamini, kumekuwa na ajenda zilizofichika na wingu la kisiasa likiwafanya wasielewa kitu gani kitatokea hapo baadaye. Wafanyakazi wengi wanachohitaji ni ukweli wa mambo. Kufanya kazi kama zamani hakuwezekani kwa maisha ya sasa, wanahitaji viongozi wao kuwasaidia kuweza kufikia malengo. Viongozi wengi wanafanya kazi ili waishi hivyo basi hawana ushawishi waliokuwa nao zamani, hivyo viongozi wasipowasaidia wafanyakazi wao kukua kitaaluma. Wafanyakazi hao wasipopata msaada huangalia njia zao binafsi na kufanya mambo kivyao.
Haya ni mambo saba ambayo imekuwa vigumu wafanyakazi kuwaamini Mabosi(viongozi) wao.

1. Kukosekana kwa ujasiri kwa viongozi wenyewe
Viongozi wengi hawana ujasiri wa kusimamia maamuzi nataratibu za majukumu yao. Wengi wao hawajui kwamba wafanyakazi wao hufuatilia nyendo na tabia zao, ingawa heshima na imani kwa kuongozi wako inategemea na kiongozi wako ana hulka gani na tabia gani kutokana na mazingira ya kazi na nje ya mazingira ya kazi.

2. Viongozi kuwa na ajenda za siri ambazo zimekaa kisiasa
. Wafanyakazi wengi wanapenda kufuata viongozi ambao si wanasiasa bali ambao wanatimiliza malengo na makusudi ya wajibu wao.


3. Ubinafsi wa ufanyaji maamuzi hufanya wafanyakazi kutowaamini viongozi wao, hivyo kutojua makusudio ya maamuzi hayo.Viongozi wanapojitizama wao wenyewe na kutokuwa na mpango unaoeleweka katika kuboresha mazingira ya kazi na kuwaendeleza walio chini yao huvunja na kuhalibu utendaji kazi wa wafanyakazi.

4. Umaarufu kupungua, kiongozi anapopoteza umaarufu vile vile imani kwa wale anaowaongoza hupua pia.

5. Tabia zisizoeleweka au kutokuwa na msimamo kitabia. Watu wengi wasiokuwa na tabia nzuri huwaamini watu wenye tabia nzuri, kwakuwa ni vigumu kufanya kazi na mtu ambaye unajua tabia yake si nzuri. Hivyo hivyo wafanyakazi hupoteza morali ya kufanya kazi na hushindwa kuwaamini viongozi wao.

6. Viongozi wasio chafua mikono yao na kujiingiza kwenye biashara, ingawa wanaongoza. Viongozi wengi hupenda kuwaachia watu wengine wafanye majukumu yao, huwafanya wafanyakazi kuhoji na kujiuliza kama kiongozi wao anajua majukumu yake. Minong’ono huanza na kutomwamini huibuka miongoni mwa wafanyakazi. Ingawa si kwamba kiongozi anatakiwa kuwa na majibu yote bali aonyeshe utendaji wake kwa anaowaoongoza ili aweke vigezo ambayo wafanyakazi watafuata. Kiongozi asiyetaka kuchafuka, nafasi yake kwa anaowaongoza hushuka.

7. Kukosekana kwa malengo. Kiongozi anapokuwa hana malengo mazuri nay a dhati kwenye ofisi aliyopo ni vigumu kuaminika.Ukiona kiongozi wako au bosi wako hana shukrani na kuthamini mchango wako katika kampuni au shirika ulilopo, yeye amekazana kukukandamiza husababisha mfanyakazi kupoteza utendaji makini kazini. Itakuwa vigumu kumwamini kama malengo yake ni kuongeza kasi ya utendaji na ushirikiano. Wafanyakazi hawapendi kuchukuliwa kana kwamba wao ni kitu cha kawaida, wanapenda kuheshimiwa, wanapofanya vizuri kupongezwa hivyo huongeza imani kwa shirika na uongozi wake.
Hayo ni mazingira saba nimejaribu kuyaainisha ingwawa kuna vitu vingi hutokea, endelea kufuatilia makala zetu uongeze ufanisi kazini kwako, na uboreshe taaluma yako kila siku.

bongo 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>