Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephine, akiwa ndani ya wodi namba moja katika Hospitali ya mkoa ya Ligula, alipokwenda kuwaona majeruhi wa ajali ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mustafa Sabodo, iliyotokea leo katika barabara ya Mtwara Lindi wakati wanafunzi wa shule hiyo wakikimbia mchakamchaka asubuhi. Kushoto Kaimu Katibu tawala wa Mkoa, Smythies Pangisa. Katika ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Masdz Benzi lenye namba za usajili T174 AEB imesababisha vifo vya wanafunzi wanne na wengine 47 kujeruhiwa
Mmoja wa majeruhi akipelekwa wodini baada ya kupokelewa katika hospitali hiyo
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kamanda wa Polisi, Zelothe Steven akizungumzia ajali hiyo