Sherehe za mapinduzi ya Zanzibar zilivyofana New York , Sherehe hizo zilipendezeshwa kwa show ya mavazi, chakula na music wa Asili ya mwambao kutoka kwa Dj Bilal. Balozi wa kudumu wa umoja wa mataifa New York Mh. Tuvako N. Manongi ndiyo alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hizo. Na alitoa hotuba fupi juu ya history ya mapinduzi. Na mama Ashura Babu pia kama ilivyo kwa Mh. Balozi Manongi alipata fulsa ya kuelezea mapinduzi hayo ya Zanzibar kwa ufupi.
Katibu wa community ya Watanzania New York bwana Mhella akitoa hotuba fupi ya kuwatambulisha viongozi na kuwakaribisha ukumbini hapo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mh. Balozi Tuvako Manongi akiongea historia fupi ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe hio
Aunt Ashura Dualle nae akitoa hotuba fupi juu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aunt Ashura anakumbukumbu sahii ya Sherehe hizo kwa sababu alikuwa mke wa marehemu mwanamapinduzi hayo Abdulhaman Babu.
Mwenyekiti wa community ya Watanzania New York bwana Hajji Khamis akimtambulisha kiongozi wa Zanzibar Diaspora kabla ya Mh. Balozi kuongea.
Naibu katibu wa Community Mariam Abu akiongea
Wageni waalikwa kutoka New York Life Insurance Comapny wakielezea umuhimu wakujiunga na Bima ya maisha.
Bwana Amani Kitali akizungumzia mambo ya maendeleo yanayotakiwa kufanywa na Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchi za nje. |