Familia ya Isaack Mruma ikiwa katika ibada maalum ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT, Usaharika wa Mbezi Beach Dar es Salaam.
Mwili wa Mtanzania Jerry Isaack Mruma aliyekuwa akisoma Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) tawi la Nairobi nchini Kenya akichukua Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) aliuawa wakati akitoka kwenye hafla ya usiku wa Mtanzania mjini Nairobi. Mwili wake ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita. Amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Mtanzania Jerry Isaack Mruma aliyekuwa akisoma Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) tawi la Nairobi nchini Kenya akichukua Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) aliuawa wakati akitoka kwenye hafla ya usiku wa Mtanzania mjini Nairobi. Mwili wake ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita. Amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mama mzazi wa Jerry, Bi Joyce Mruma, Khan Mruma ambaye ni kaka wa marehemu, baba mzazi wa Jerry, Isaack Mruma na mdogo wake Kelvin Mruma wakiwa katika ibada hiyo.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika ibada hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Assah Mwambene akipita kutoa heshima za mwisho.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkomwa akipita kutoa heshima za mwisho.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN, Gabriel Nderumaki akitoa heshima za mwisho.
Ndugu jamaa na marafiki wakitoa heshima za mwisho.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Goodluck Ole Medeye akitoa heshima za mwisho.
Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia) akimfariji Isaack Mruma kwa msiba wa mtoto wake.
Cleopa David Msuya akimfariji mama wa Jerry, Joyce kwa msiba wa mwanae.
Mama mzazi wa Jerry akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mwanae.
Isaack Mruma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mtoto wake Jerry Mruma.
Ilikuwa ni vilio kwa ndugu na jamaa wa familia ya Mruma.
Mwili ulitolewa Kanisani na safari ya Makaburini Kinondoni ilianza.
Mwili wa Marehemu Jerry ukifikishwa makaburini.
Ni majonzi sana...Isaack Mruma akimfariji mkewe Joyce Mruma kwa msiba huo wa mtoto wao.
Sanduku lilishushwa kaburini
Kelvin akimfariji mama yake.
Hakika ni majonzi sana kwa familia hii...na Mungu daima aliwapa nguvu na kuendelea na safari ya mwisho ya mpendwa wao.
Wazazi wakiweka udongo katika kaburi
Nimajonzi yalikuwa kwa kila mtu...
mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walioshudhuria mazishi hayo.
Mafundi wakifanya yao...
familia ya ikiwa makaburini.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Goodluck Ole Medeye akiweka shada.
Prof. John Nkoma wa TSRA akiweka shada.
Pudensiana Temba akiweka shada la maua kwaniaba ya Staff wa TSN.