Juzi Kati ndani ya studio za Sibuka FM,Katika kipindi cha Pepeta Afrika, mgeni rasmi nyota wa wiki alikuwa kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi maarufu barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni,aka Anunnaki Alien au "Watoto wa Mbwa". Kamanda Ras Makunja alifanya maohijiano ya TV na Redio Sibuka, na alizungumuzia zaidi nafasi ya muziki wa dansi wa Tanzania katika masoko ya kimataifa,
Mwanamuziki huyo wa Tanzania mwenye makao yake nchini Ujerumani alitoa wito kwa watanzania waishio ndani na nje ya Tanzania kuzipa nafasi bendi za muziki za Tanzania ili ziweze kuvusha muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania ,pia kufanya tour za kimataifa.
Ras Makunja aliutaja muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" kuwa una nafasi kubwa katika soko la kimataifa hiwapo Watanzania wenyewe watakuwa mstari wa mbele katika kuutanga na kuzipendekeza bendi za Tanzania kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho ya kimataifa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katika studio za Sibuka FM,jijini Dar-es-salaam Ras Makunja aliongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Komandoo Hamza Kalala ambaye aliutaja muziki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kuwa ni muziki ulipangiliwa kwa mtindo wa kushambulia na kuteka washabiki katika masoko.
Komando Hamza Kalala alimtaja Kamanda Ras Makunja kuwa ni mojawapo wa wanamuziki wachache wa kitanzania wanao ipeperusha bendera ya Bongo kimataifa bila ya uwoga.
Usikose kuwasikiliza FFU wa Ngoma Africa band at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com. Jiunge nao at www.facebook.com/ ngomaafricaband