Sehemu ya Kwanza..
Kama ada kama dawa blog yetu inajieleza kwamba itakuwa inakumbusha au kutoa elimu ya vitu tunavyovijua lakini tumesahau au hatufuatilii, nah ii yote ni kutaka kukupa changamoto wewe msomaji ili uweze kufikiri njia nyingine ya kuweza kujiongezea kipato kupitia kilimo pia.
Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora zaidi.
Kwenye shamba la bwana Buberwa Robert, atakuwa na kitalu chenye zaidi ya miche 1500 ya miparachichi, ikiwa inasubiri kufikia wakati wa kupandikiza.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFA HAPA CHINI
Mbinu anayotumia
Kukusanya kokwa za parachichi kutoka maeneo ya sokoni; atakachofanya ni kuhakikisha tu kuwa mbegu hiyo ni safi, haijaathiriwa na magonjwa na itaota. Baada ya hapo huchagua zile zenye muundo mzuri na kuzipanda kwenye boksi au kwenye sehemu ya kitalu. Baada ya kuota ataziotesha kwenye makopo, au kwenye viriba kisha kuendelea kumwagilia maji mpaka zinapokuwa na umbo usawa wa penseli. Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati mmea umefikisha unene wa penseli. Kupandikiza kwa kutumia chipukizi lililolingana na mche unaopandikizia ni njia yenye mafanikio zaidi.
Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati ambao mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa kupandikiza ni lazima lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na ni lazima umbo liwiane na mti linapopandikizwa kuzuia maji yasipotee na kusababisha pandikizi kukauka.
Mapandikizi ni lazima yatokane na aina ya parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile HASS, FUERTE au PUEBLA . Kwa wale wakulima ambao mmea utatoa majani mapya. wana mkataba na Africado, watahitaji kupata mapandikizi kutoka kwenye miti ya HASS. Hii ina maanisha kuwa mkulima anayetaka kuanzisha kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande walau miti 5 ya parachichi aina ya HASS ili kupata mapandikizi.
Njia ya kupandikiza ina ufanisi zaidi na ni rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini ya asilimia 75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo inastahimili magonjwa. Wakulima pia wamekuwa na rekodi nzuri ya ongezeko la mavuno kutokana na mimea waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa matumizi ya madawa.
Wakulima ambao wanafanya kazi zao chini ya CARITAS Njombe sasa wanaona faida kubwa inayotokana na kupandikiza, wameamua kuwekeza kwenye utaalamu huu na kuwa na miche mingi kwenye vitalu vyao. Hii ni mbinu ya kilimo ambayo ina faida kubwa kwa mkulima, huku akiwa amewekeza kwa kiasi kidogo sana katika kukabiliana na wadudu na magonjwa na kuepuka kuwa na mazao yenye ubora wa chini.
Usikose sehemu ya Pili ambapo Tutagusia zaidi katika suala zima la Namna ya Kupanda Parachichi, Faida na utapataje Kipato katika tunda hili usikose